Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne zataka saini ya Feisal Zanzibar

FEISAL Pict

Muktasari:

  • Tetesi zilizopo kwasasa, mshambuliaji huyo alishamaliza mkataba na timu hiyo lakini bado inahitaji kumpa mkataba mpya ingawaje hajafanya uamuzi.

MSHAMBULIAJI wa JKU, Feisal Hilali 'Feymar' ameziweka timu nne mezani ambazo zote zinahitaji huduma yake huku moyo wake ukibaki JKU.

Tetesi zilizopo kwasasa, mshambuliaji huyo alishamaliza mkataba na timu hiyo lakini bado inahitaji kumpa mkataba mpya ingawaje hajafanya uamuzi.

Wakati hali ikiwa hivyo, Mlandege, Zimamoto na Black Sailors, zimeingia vitani kuwania saini yake.

Baada ya kusikia tetesi hizo, Mwanaspoti ilimtafuta mshambuliaji huyo ambapo amesema kwa sasa bado hajafanya uamuzi lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kuitumikia JKU.

"Ni kweli hizo timu zinahitaji huduma yangu lakini bado sijafanya uamuzi wowote hadi kufikia sasa," amesema.

Alifafanua kuwa, mkataba baina yake na JKU umemalizika lakini wapo katika mazungumzo ya kuongeza.

Wakati Feisal akiendelea kujishauri kuongeza mkataba, chanzo cha ndani ya timu hiyo kimemuambia mwandishi wa habari hii kuwa wachezaji wa timu hiyo hawahitaji kusaini timu nyingine ya Zanzibar zaidi ya kutoka nje na kama kubaki, bora waendelee kusalia hapo kwani kuna maslahi mazuri.

Chanzo hicho kimesema timu hiyo haina ubabaifu wa posho kwa wachezaji wake ndio sababu ya wengi kubaki na viongozi wanaishi nao kwa upendo.