Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Job yuko sana Yanga 2025

Muktasari:

  • Job ambaye mkataba wake ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu amesaini mkataba huo akitangazwa rasmi Leo na kumfanya kuendelea kuwa klabuni hapo mpaka 2025.

Hatimaye Yanga imemaliza utata wa hatma ya beki wao Dickson Job baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili.

Job ambaye mkataba wake ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu amesaini mkataba huo akitangazwa rasmi Leo na kumfanya kuendelea kuwa klabuni hapo mpaka 2025.

Job amekiri kuwa ameamua kusalia Yanga licha ya kuwa na ofa nyingi kwa klabu zingine lakini amefanya maamuzi ya kusalia klabuni hapo alikojiunga msimu wa 2020/21 akitokea Mtibwa Sugar.

"Nikweli nilikuwa na ofa mbalimbali lakini baada ya tafakari ya kina nimeamua kubaki hapa Yanga, ni heshima kuendelea kuichezea klabu hii kubwa,"amesema Job ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi hicho.

Hatua hiyo ya Job kuongeza mkataba mpya utawashusha presha mashabiki wa Yanga ambao kesho timu yao itashuka uwanjani kuwa wageni wa watani wao wa jadi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Beki huyo amekuwa nguzo muhimu ndani ya Yanga tangu imsajili akiwa na uwezo wa kucheza zaidi ya nafasi Moja katika eneo la ulinzi.