Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya jezi ya Casemiro Yanga iko hivi

JEZI Pict

Muktasari:

  • Casemiro kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga ilianzia ugenini dhidi ya Namungo, jezi yake kifuani ilikuwa na jina la mdhamini mkuu wa klabu hiyo, SportPesa, ambapo alianza kikosi cha kwanza, huku timu hiyo ikishinda 3-1.

ULIONA kiungo wa Yanga, Abdulnassir Mohammed Abdallah ‘Casemiro’ ile jezi yake iliyozua gumzo baada ya kufichwa jina la mdhamini mkuu wa klabu hiyo? Basi ishu kamili iko hivi huku Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ikitajwa.

Casemiro kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga ilianzia ugenini dhidi ya Namungo, jezi yake kifuani ilikuwa na jina la mdhamini mkuu wa klabu hiyo, SportPesa, ambapo alianza kikosi cha kwanza, huku timu hiyo ikishinda 3-1.

Jana, wakati Yanga ikicheza nyumbani dhidi ya Coastal Union katika mwendelezo wa ligi hiyo aliingia kipindi cha pili, lakini jezi yake ikafichwa jina la mdhamini huyo, Yanga ikishinda tena 4-1. Hatua hiyo ikazua maswali kwa nini imekuwa hivyo.

Uongozi wa Yanga umetoa kauli juu ya hilo ambapo Ofisa Habari, Ally Kamwe ameliambia Mwanaspoti kwamba, jezi ambayo ilitumika kwenye mchezo dhidi ya Namungo, ilikuwa na makosa makubwa.

JEZ 01

Kamwe amesema, baada ya Casemiro kuvaa jezi hiyo yenye jina la mdhamini, waliandikiwa barua rasmi na TPLB, wakikumbushwa kwamba kiungo huyo hakutakiwa kuvaa jezi yenye mdhamini wao mkuu aliyepo kifuani kutokana na kuzuiwa kisheria kwa kuwa hajafikisha miaka 18.

“Nikweli jana  Casemiro jezi yake haikuwa na jina la mdhamini, huo ndio ulikuwa usahihi kwa kuwa, kijana wetu huyu hajafikisha miaka 18 na anatakiwa asitumie jezi inayotangaza michezo hii,” amesema Kamwe.

“Tulifanya makosa kwenye mchezo dhidi ya Namungo na wenzetu Bodi ya Ligi walituandikia barua na tukawaomba radhi kwa kilichotokea, ndio maana kwenye mchezo dhidi ya Caoastal Union tulibadilisha na akatumia jezi ambayo anatakiwa kutumia kikanuni kulingana na umri wake.

JEZ 02

“Kwa sasa hatavaa jezi hizo mpaka atakapofikisha umri sahihi, hii ni kwa Casemiro na vijana wote ambao tutakuwa tunawapandisha, watakaokuwa na umri chini ya miaka 18 watakuwa na jezi ambazo hazina jina la mdhamini mkuu, hili ni muhimu likaeleweka hivyo, kwa wachezaji wengine wao watazitumia jezi zao kama kawaida.”

Kanuni na sheria za michezo ya kubahatisha nchini Tanzania (chini ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura ya 41) zinazuia mtu mwenye umri chini ya miaka 18 kujihusisha na au kutangaza michezo ya kamari.

Hii inajumuisha wachezaji wadogo kutoruhusiwa kuvaa jezi zenye nembo au majina ya kampuni za kubeti.