Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaishusha Simba, ikijipigia Coastal Union

Muktasari:

  • Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi sita sawa na Simba wakitofautiana kwa mabao ya kufunga.

Yanga imeendeleza moto wake mbele ya Coastal Unioni baada ya kuichapa mabao 4-1, na kuishusha Simba kileleni mwa Ligi Kuu Bara ndani ya saa 24.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi sita sawa na Simba wakitofautiana kwa mabao ya kufunga.

Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex, mabao ya Yanga yalifungwa na Albert Kangwanda, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya na Mohamed Hussein aliyeingia akitokea benchi na kukamilisha shangwe hiyo ya mashabiki wa Yanga.

Yanga kwa ushindi huo imendeleza rekodi yake ya kuichapa Coastal, ikishinda mechi zake 13 kati ya 16 za Ligi Kuu Bara, ikifikisha jumla ya mabao 31 huku Wagosi hao wa Tanga bao lao likiwapa goli sita jumla.

Yanga ilitawala mchezo huo tangu mwanzo na kuwanyima kabisa Coastal ambao muda mwingi walitumia kujilinda huku kipa wake Chuma Ramadhan akifanya kazi kubwa kuokoa hatari  kadhaa.

Kipa huyo aliokoa mashuti sita yaYanga yaliyolenga lango, akiwabakisha mchezoni Coastal Union.

Hata hivyo jitihada za kipa huyo zilipoteza mwelekeo katika dakika ya 38, Yanga ikafanikiwa kufungua ukuta wa Coastal ikipata bao kwa shuti kali kupitia kiungo wake Albert Kangwanda akipokea pasi ya beki wake Chadrack Boka.

Kuingia kwa bao hilo kukazidi kuilainisha Coastal ikiruhusu bao la pili 45+2 likifungwa na Maxi Nzengeli kwa shuti kali akipokea asisti ya Housseine Zakouani.

Mpaka mapumziko Yanga ikatoka na uongozi wa mabao 2-0 huku ikitawala vizuri mchezo huo wakati Coastal Union ikiwa na kazi moja tu ya kuzuia ikitoka bila kupiga shuti lililolenga lango.

Kipindi cha pili Coastal ikapata pigo dakika ya 48 baada ya kiungo wake na nahodha Geoffrey Manyasi kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya Duke Abuya.

Tukio hilo limenaswa na marudio ya Video Sapoti (FVS) yaliyomwezesha mwamuzi Raphael Ikambi kutoka Morogoro kuona tukio hilo.

Dakika mbili baadaye Yanga ikapata bao la tatu likifungwa na kiungo Mudathir Yahaya kwa shuti akimalizia pasi ya beki Yao Kouassi.

Mshambuliaji Peter Shalulile alifanikiwa kufunga mabao mawili, lakini yakakataliwa kupitia marudio ya Video sapoti.

Coastal Union ikafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 77 kupitia kiungo wake Gradi Kiala, kwa mpira wa adhabu baada ya shuti lake kumgonga beki wa Yanga, Boka kwenye ukuta, na kumpoteza kipa wa timu hiyo Djigui Diarra.

Beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' akapigilia msumari wa nne akifunga bao la mwisho kwa krosi ambayo ilijaa moja kwa moja wavuni na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Yanga kushinda kwa mabao 4-1.