Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge avuta pumzi Azam, amkingia kifua Manula

IBENGE Pict

Muktasari:

  • Raia huyo wa DR Congo, amebainisha kwamba, pia kitendo cha kipa wa kikosi hicho, Aishi Manula kuonyeshwa kadi nyekundu, hana sababu ya kumlaumu.

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema ushindi dhidi ya TRA United umeipa nguvu timu hiyo kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Pamba Jiji, huku akifichua kuwa bado ana kibarua cha kuendelea kuboresha kikosi hicho kutokana na ugumu wa ratiba.

Raia huyo wa DR Congo, amebainisha kwamba, pia kitendo cha kipa wa kikosi hicho, Aishi Manula kuonyeshwa kadi nyekundu, hana sababu ya kumlaumu.

Azam ilipata ushindi wake wa kwanza wa msimu huu wa 2026-2027 baada ya kuichapa TRA United mabao 2-1, katika mchezo ambao Ibenge amekiri ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Ibenge amesema alifahamu mapema kuwa mchezo huo ungekuwa na ushindani mkubwa, akieleza kuwa wapinzani wao ni miongoni mwa timu zinazocheza soka zuri nchini na zina mtindo unaofanana kwa kiasi kikubwa na Azam.

AZA 01

“Nilisema kabla ya mchezo kwamba wao ni moja ya timu bora Tanzania. Wanacheza vizuri, wanacheza soka zuri na wanafanana nasi kwa namna wanavyocheza. Wanashambulia kama sisi na wanajilinda kama sisi,” amesema.

Ibenge pia tofauti kubwa kati ya mchezo huo na uliopita ilikuwa aina ya wapinzani pamoja na mazingira ya mchezo, akibainisha kuwa Azam imeendelea kupata muda zaidi wa mazoezi ambao umeisaidia kuboresha baadhi ya mambo.

Amesema ratiba ya msimu huu ni ngumu kutokana na timu kucheza michezo ndani ya muda mfupi, hivyo wachezaji wanapaswa kuwa tayari kimwili na kiakili.

AZA 02

Kocha huyo amewataka pia mashabiki wa Azam kuendelea kuwaunga mkono katika michezo inayofuata, akisema uwepo wao unaweza kuongeza nguvu kwa wachezaji.

“Tunacheza Jumapili, hivyo tunawahitaji mashabiki wetu. Michezo yote msimu huu itakuwa migumu na ratiba ni fupi. Tunacheza kila baada ya siku tatu au nne, kwa hiyo tunahitaji sapoti yao ili kutupa nguvu zaidi ya kwenda kushinda,” amesema.

Akizungumzia kadi nyekundu ya Manula aliyoonyeshwa dakika ya 77, Ibenge amesema kipa huyo alijitoa muhanga katika kulinda lango lake lisiguswe, lakini bahati mbaya akafanya faulo.

AZA 03

Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa TRA United, Ousmane Kamisoko, alifanikiwa kupenya ngome ya ulinzi ya Azam na kumkuta Manula ambaye alilazimika kumchezea faulo akiwa anakaribia kufunga bao la kusawazisha. Wakati huo Azam ilikuwa inaongoza 2-1.

“Manula alijitoa muhanga kwa ajili ya timu. Kama asingefanya vile, TRA ingerudisha goli. Lakini kwa akili yake na maamuzi yake magumu, Azam ikabaki salama na tukaweza kushinda mchezo,” amesema Ibenge.