Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yaichapa TRA, rekodi yatibuliwa

AZAM Pict

Muktasari:

  • TRA United imekuwa timu ya kwanza kutikisa nyavu za Azam kwenye uwanja wake wa nyumbani katika Ligi Kuu Bara baada ya mechi 17 mfululizo ambazo kikosi hicho cha Chamazi kilimaliza bila kuruhusu bao, rekodi iliyodumu tangu Aprili 10, 2025.

AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Alhamisi, Agosti 20, 2026, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, lakini ushindi huo umeacha doa kwenye rekodi yake ya muda mrefu ya kutoruhusu bao nyumbani.

TRA United imekuwa timu ya kwanza kutikisa nyavu za Azam kwenye uwanja wake wa nyumbani katika Ligi Kuu Bara baada ya mechi 17 mfululizo ambazo kikosi hicho cha Chamazi kilimaliza bila kuruhusu bao, rekodi iliyodumu tangu Aprili 10, 2025.

AZA 01

MCHEZO ULIVYOKUWA
Azam ilianza mchezo kwa kasi na ilipata bao la kuongoza dakika ya nane kupitia Idd Seleman 'Nado', aliyefumua shuti kali la mguu wa kushoto nje ya boksi baada ya mpira kuokolewa kwa kichwa na TRA United kufuatia kona.

Wenyeji waliendelea kulisakama lango la TRA United na juhudi zao zilizaa bao la pili dakika ya 34. Pascal Msindo alitengeneza krosi kutoka upande wa kushoto iliyounganishwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ kwa mguu wa kushoto na kumshinda kipa, Daniel Mgore.

Azam ikaenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

TRA United ilirejea kipindi cha pili ikiwa na sura mpya baada ya kocha Etienne Ndayiragije kufanya mabadiliko mawili, akiwaingiza Emmanuel Mwanengo na Ousmane Kamissoko kuchukua nafasi za Greyson Gwalala na Steve Belobo.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda haraka kwani sekunde ya 25 tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Kamissoko alifunga kupitia mpira wake wa kwanza kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Ani Prince Elijah, akiifungia TRA United bao.

Bao hilo liliwapa wageni nguvu mpya na kuanza kuisakama Azam, huku Aishi Manula akilazimika kufanya kazi ya ziada kulinda lango lake.

AZA 02

Dakika ya 68, Manula alifanya uokoaji muhimu baada ya shambulizi la Emmanuel Mwanengo kutishia kuzaa bao la kusawazisha.

Ndayiragije aliendelea kufanya mabadiliko, akiwatoa Tobias Omondi na Ani Elijah na kuwaingiza Dzaba Vicent na Kassim Shaibu.

Azam nayo ilifanya mabadiliko dakika ya 72, Donovan Makoma akampisha Yahya Zayd, huku Sopu akitoka na Nassor Saadun kuingia.

Hata hivyo, mchezo ulibadilika zaidi dakika ya 77 baada ya Manula kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Kamissoko nje ya boksi wakati mshambuliaji huyo wa TRA United akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga.

Kocha wa Azam, Florent Ibenge alilazimika kumtoa kiungo, Abdulkarim Kiswanya na kumuingiza kipa wa akiba, Hamis Athuman ili kulinda lango la Azam katika dakika zilizobaki.

Licha ya kucheza pungufu kwa takribani dakika 13, Azam ilifanikiwa kuhimili presha ya TRA United na kulinda ushindi wa mabao 2-1.

Ushindi huo umeifikisha Azam pointi nne na kuiweka nafasi ya tano kwenye msimamo. Yanga ipo kileleni na pointi sita kama ilizonazo Simba, huku Singida Black Stars na Polisi Tanzania zikiwa na pointi nne pia.

AZA 03

REKODI YAVUNJWA
Kabla ya mchezo wa leo, Azam ilikuwa haijaruhusu bao nyumbani katika Ligi Kuu Bara kwa mechi 17 mfululizo, tangu ilipopoteza 2-1 dhidi ya Yanga, Aprili 10, 2025.

Katika mechi hizo 17, Azam ilishinda 13 na kutoka sare nne, huku ikifunga mabao 36 bila nyavu zake kutikiswa.

Mfululizo huo ulianza kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji Mei 13, 2025, ukafuatiwa na ushindi wa 5-0 dhidi ya TRA United Juni 18, 2025.

Azam iliendelea na rekodi hiyo dhidi ya Mbeya City (2-0), Singida Black Stars (0-0), Coastal Union (3-0), Fountain Gate (0-0), TRA United (2-0), Mtibwa Sugar (3-0), Yanga (0-0), Simba (0-0), JKT Tanzania (3-0), Namungo (1-0), Pamba Jiji (2-0), Tanzania Prisons (2-0), KMC (3-0), Mashujaa (2-0) na Dodoma Jiji (3-0).

Licha ya Azam kupata pointi zote tatu, lakini TRA United imeandika historia kwa kuwa timu ya kwanza kuvunja ukuta wa timu hiyo ya kucheza mechi 17 za Ligi Kuu Bara bila kuruhusu bao ikiwa nyumbani.