Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hussein Kazi aibukia singida Black Stars

KAZI Pict

Muktasari:

  • Kazi amejiunga na Singida Black Stars kwa mkataba wa miaka miwili, huku akieleza kuwa moja ya sababu zilizomvutia kujiunga na timu hiyo ni ushiriki wake katika michuano ya kimataifa.

SINGIDA Black Stars imekamilisha usajili wa beki wa kati, Hussein Kazi, aliyekuwa akiitumikia Namungo FC msimu uliopita wa 2025-2026, akicheza kwa kiwango cha juu katika kikosi cha kwanza.

Kazi amejiunga na Singida Black Stars kwa mkataba wa miaka miwili, huku akieleza kuwa moja ya sababu zilizomvutia kujiunga na timu hiyo ni ushiriki wake katika michuano ya kimataifa.

Namungo awali ilimtangaza Kazi kuwa angeendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2026-2027, ambao umeanza leo Agosti 14, 2026, lakini beki huyo ameamua kuhamia Singida Black Stars.

KAZ 01

Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Kazi amesema mazungumzo yake na Namungo yalikuwepo, lakini hakusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

“Ni kweli tulikuwa kwenye mazungumzo na Namungo ili niendelee kusalia katika timu hiyo, lakini sikusaini ndiyo maana uliona kuna wakati waliniweka kwenye orodha ya wachezaji wao,” amesema Kazi.

Ameongeza: “Singida BS inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo nitapata nafasi ya kucheza jambo ambalo linatamaniwa na kila mchezaji.”

Kazi anawasili Singida Black Stars akiwa na rekodi nzuri ya msimu uliopita, ambapo alicheza mechi zote 30 za Ligi Kuu ya NBC, akiitumikia Namungo kwa jumla ya dakika 2,700.

Kabla ya kujiunga na Namungo, Kazi aliwahi kuitumikia Simba kwa misimu miwili (2024-2024 na 2024-2025), baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Geita Gold.

KAZ 02

Usajili wake unaongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya Singida Black Stars, ambayo msimu huu inatarajia kushiriki pia katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa msimu wa 2026-2027, kikosi cha Singida Black Stars kitakuwa na wachezaji 31 ambapo makipa ni Metacha Mnata, Athuman Ismail na Yona Amos.

Mabeki; Frank Assinki, Benjamin Tanimu, Said Hemed, Ibrahim Imoro, Ande Koffi, Rahim Shomari, Miraj Abdallah, Kennedy Juma, James Mwashinga, Hussein Kazi na Abdulmalick Zakaria.

Viungo; Emmanuel Keyekeh, Marcel Canadi, Seydou Sacko, Dramane Kambou, Deus Kaseke, Idd Hussein Kanyika, Ladack Chasambi, Ahmed Pipino, Omary Abdallah, Abdallah Hamis na Sheikhan Khamis.

Washambuliaji; Mathew Tegisi, James Mboma, Yusuph Hamis, Andrew Simchimba, Exauce Nzao na Jonathan Sowah.