Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hemed Morocco aichukua Junguni

Muktasari:

  • Katika kuhakikisha Junguni United inafanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza Pemba na kurudi Ligi Kuu Zanzibar, taarifa kutoka kisiwani humo zinaeleza, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania maarufu Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amechukua timu hiyo na sasa ni mmiliki halali.

BAADA ya Junguni United kushuka daraja msimu uliopita wa 2025-2026 kutoka Ligi Kuu Zanzibar na kufanya mabadiliko ya uongozi kwa kumuondosha aliyekuwa katibu wa timu hiyo, Suleiman Mwidani, sasa imekuja kivingine.

Katika kuhakikisha Junguni United inafanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza Pemba na kurudi Ligi Kuu Zanzibar, taarifa kutoka kisiwani humo zinaeleza, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania maarufu Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amechukua timu hiyo na sasa ni mmiliki halali.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo, kililiambia Mwanaspoti, Kocha Morocco analenga kuirejesha Junguni United kushiriki Ligi Kuu Zanzibar, huku pia akipanga kuihamishia kisiwani Unguja kutokea Pemba.

Mtoa taarifa huyo aliendelea kueleza hivi sasa Kocha Morocco yupo kisiwani Pemba akiwa na jukumu la kuweka mikakati mizuri kuhakikisha timu hiyo inakuwa na maandalizi bora ya Ligi Daraja la Kwanza, katika hilo, amefika kukagua uwanja wa kufanyia mazoezi, huku pia akitafuta wachezaji wa kuongeza nguvu kikosini.

“Kocha Morocco ndio bosi wa Junguni kwasasa na yupo Pemba anatafuta wachezaji, pia amefika kukagua uwanja wa mazoezi,” kilisema chanzo hicho.

Ingawa mwenyewe na viongozi wa klabu hiyo hawataki kuzungumzia ukweli wa taarifa hizo, lakini Mwanaspoti linafahamu, Kocha Morocco aliandaa bonanza lililofanyika Agosti 15, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba, likiwa na lengo la kusaka vipaji kuanzia umri wa miaka 17 hadi 23 ili kuchagua wachezaji watakaoisaidia timu hiyo kufikia malengo.

“Hemed Morocco anasimama kama bosi wa timu, amekuja na kocha Ali Ameir ambaye huyo ndiye atakayeiongoza Junguni katika kipindi chake,” kilisema chanzo hicho.

Kocha Ali Mohamed Ameir ambaye anatajwa kuwa ataiongoza Junguni United, amewahi kuifundisha Coastal Union msimu wa 2025-2026, huku akiiongoza timu hiyo katika mechi tatu pekee za Ligi Kuu Bara kabla ya kusitishiwa mkataba wake.