Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola Mnene aipa neno ZFF

MGUNDA Pict

Muktasari:

  • Amesema, endapo Ligi ya Vijana itaboreshwa kwa kutafutiwa wadhamini, hilo litaipa nguvu Ligi Kuu Zanzibar na itakuwa sababu ya kuongezeka kwa ushindani.

KOCHA Hassan Makame ‘Guardiola Mnene’ amelishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kuwekeza ngazi ya vijana kwa lengo la kuviendeleza vipaji vyao.

Amesema, endapo Ligi ya Vijana itaboreshwa kwa kutafutiwa wadhamini, hilo litaipa nguvu Ligi Kuu Zanzibar na itakuwa sababu ya kuongezeka kwa ushindani.

Amesema, mambo hayo yataisaida ZFF kupata uanachama wa FIFA ili Zanzibar ipate nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia.

“Naishauri ZFF wakuze mpira ngazi ya vijana kwa kutafuta wadhamini kuboresha ligi kuanzia vijana hadi Ligi Kuu Zanzibar ili watafute uanachama wa FIFA ili na sisi tupate kushiriki mashindano makubwa kama Kombe la Dunia,” amesema.

Kocha huyo ambaye msimu uliopita alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la KVZ iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, amesema msimu ujao hatakuwa sehemu ya kikosi hicho.

Amesema, hadi sasa zipo ofa tatu ya timu zinazohitaji huduma yake ingawa hajafanya uamuzi.