Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamera apata matumaini Chipukizi

GAMERA Pict

Muktasari:

  • Katika michezo mitano iliyosalia kumaliza mzunguko wa kwanza, Chipukizi itakutana na Mafunzo, KMKM, KVZ, Polisi na Wembe.

KOCHA Mkuu wa Chipukizi, Suleiman Mohammed ‘Mani Gamera’, amesema kwa sasa anaridhishwa na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo, ingawa bado anahitaji kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo.

Amesema katika mwezi Oktoba, Chipukizi imeonesha kiwango kizuri kilichompa matumaini ya kufanya vizuri katika michezo mitano iliyosalia kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Zanzibar.

Katika mechi nne ilizocheza mwezi huo, Chipukizi ilishinda mbili dhidi ya Fufuni kwa bao 1-0 na Raskazone kwa mabao 2-1. Pia, ilitoka sare ya bila kufungana na Mwenge, huku ikipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Muembe Makumbi.

Gamera amesema timu hiyo imeanza kuimarika, ikiwemo kupunguza idadi ya mabao inayofungwa, jambo linalorejesha matumaini ya kufanya vizuri katika michezo ijayo.

“Timu imeanza kunipa matumaini ya kufanya vizuri na kuna baadhi ya maeneo nitayaboresha kuelekea usajili wa dirisha dogo,” amesema.

Baada ya kucheza mechi 10, Chipukizi inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na ushindi mara tatu, sare mbili na vipigo vitano.

Katika michezo mitano iliyosalia kumaliza mzunguko wa kwanza, Chipukizi itakutana na Mafunzo, KMKM, KVZ, Polisi na Wembe.

Gamera amesema anatambua kuwa michezo hiyo haitakuwa rahisi, lakini amejipanga kuhakikisha timu yake inakabiliana vyema na wapinzani wake ili kupata matokeo mazuri.