Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamera akomalia utimamu Chipukizi

Muktasari:

  • Gamera alisema, kikosi hicho kimeanza mazoezi kwa ari mpya, kikilenga kujenga msingi imara wa msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa visiwani hapa.

KOCHA Mkuu wa Chipukizi, Suleiman Mohammed ‘Mani Gamera’ amesema timu hiyo ipo katika mazoezi ya kujiandaa na msimu wa 2026-2026 huku akisisitiza kurejesha utimamu wa mwili na kuwaandaa wachezaji kiushindani.

Gamera alisema, kikosi hicho kimeanza mazoezi kwa ari mpya, kikilenga kujenga msingi imara wa msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa visiwani hapa.

Alisema, wanafahamu kwamba ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar inaonyesha timu hiyo itaanza kwa kucheza mechi zake kisiwani Unguja, hivyo maandalizi yanaendelea kuhakikisha anaanza vizuri.

“Naendelea kutathmini uwezo wa kila mchezaji ili kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa, lakini kubwa zaidi nataka utimamu wa mwili kwa wachezaji umekuwa sawa, pia ushindani ndani ya timu uwepo kwani hiyo ndiyo sehemu muhimu ya maandalizi ya kikosi,” alisema Gamera.

Kocha huyo ambaye msimu uliopita aliinoa Fufuni, alisema Chipukizi inalenga kuanza msimu mpya ikiwa na kikosi imara, chenye umoja na nidhamu, huku malengo makubwa yakiwa ni kufanya vizuri katika Ligi Kuu Zanzibar.

Alisema, mpango wa kufanya vizuri utaanzia kambini ambapo nidhamu, umoja na utekelezaji wa maelekezo ya benchi la ufundi vitakuwa nguzo muhimu katika safari ya timu kuelekea msimu mpya.

Alibainisha kuwa, lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kila mchezaji anapambana kuonyesha uwezo wake mazoezini na kumshawishi kuwa anastahili kuanza katika kikosi cha kwanza.