Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamera azimia, Chipukizi ikiichapa mlandege

GAMERA Pict

Muktasari:

  • Hali hiyo ilimpata dakika ya 65 ya mchezo ambao Chipukizi iliikaribisha Mlandege uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Hata hivyo, Chipukizi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa mapema dakika ya tisa na Ismail Said.

KATIKA hali isiyotarajiwa, Kocha Mkuu wa Chipukizi United, Suleiman Mohamed’ Gamera’ amezimia uwanjani ghafla baada ya mchezaji wa timu hiyo, Ali Mwadini kukosa bao la wazi.

Hali hiyo ilimpata dakika ya 65 ya mchezo ambao Chipukizi iliikaribisha Mlandege uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Hata hivyo, Chipukizi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa mapema dakika ya tisa na Ismail Said.

Kutokana na tukio hilo, viongozi wa timu hiyo na benchi la ufundi walilazimika kumuondosha uwanjani na kumpeleka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kupata huduma ya kwanza.

Kocha huyo alikuja kupata utimamu wa mwili baada ya mechi hiyo kumalizika na hadi sasa anaendelea vizuri.

Mwanaspoti linatambua, hali hiyo ilitokana na kocha huyo kukosa ushindi katika mechi nne za Ligi Kuu Zanzibar zilizopita kabla ya kuichapa Mlandege kwani ilipoteza tatu na sare moja dhidi ya Black Sailors.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtunza Takwimu Mkuu wa Chipukizi United, Suleiman Rajab Othman amesema Gamera kwa sasa anaendelea vizuri kwani alipata mshtuko kidogo akiwa uwanjani.

“Alipata mshtuko wa kawaida tu lakini kwasasa anaendelea vizuri,” amesema Othman. Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa Gamera tangu atue kuinoa Chipukizi United msimu huu ambapo sasa timu hiyo imefikisha pointi nne ikikamata nafasi ya 12 kabla ya mechi za jana.