Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate yaendelea kusuasua Ligi Kuu

MBEYA Pict
MBEYA Pict

Muktasari:

  • Shujaa wa Mbeya City katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji Oscar Mwajanga ambaye ndiye alipachika mabao yote mawili.

FOUNTAIN GATE imeendelea kuwa na matokeo ya kusuasua kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa mabao 2-0,  kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Shujaa wa Mbeya City katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji Oscar Mwajanga ambaye ndiye alipachika mabao yote mawili.

Mwajanga alifunga bao la kwanza katika dakika ya 84 na bao la pili alipachika katika dakika ya 86, mabao ambayo yameipa matokeo mazuri Mbeya City na kuifanya ipande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tisa.

Mabao hayo pia yamemfanya Mwajanga awe amepachika mabao matatu msimu huu na hivyo kuwa miongoni mwa vinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Ni matokeo yaliyoendeleza wimbi la matokeo mabaya kwa Fountain Gate ambayo sasa imepoteza michezo mitatu kati ya minne iliyocheza hadi sasa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Felix Minziro, imeshinda mechi moja tu na hivyo ina pointi tatu.

Baada ya mechi ya leo, mchezo unaofuata wa Fountain Gate utakuwa ni dhidi ya Yanga ambao utachezwa Septemba Mosi, mwaka huu katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mbeya City yenyewe katika mchezo unaofuata itakuwa katika Uwanja huohuo dhidi ya TRA United.