Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Simba kuivamia Mighty Wanderers

Muktasari:

  • Simba baada ya mchezo wake dhidi ya Geita Gold, itaelekea nchini Malawi kuanza kampeni yake ya kuisaka fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu 2026-2027 itakapoikabili Mighty Wanderers, Septemba 6, 2026, mchezo ukitarajiwa kupigwa Uwanja wa Bingu jijini Lilongwe.

MBEYA; WAKATI Simba ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold utakaochezwa Agosti 31, 2026, mashabiki wa timu hiyo jijini Mbeya wameanza hesabu za kuwavamia wapinzani wao kimataifa, Mighty Wanderers katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba baada ya mchezo wake dhidi ya Geita Gold, itaelekea nchini Malawi kuanza kampeni yake ya kuisaka fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu 2026-2027 itakapoikabili Mighty Wanderers, Septemba 6, 2026, mchezo ukitarajiwa kupigwa Uwanja wa Bingu jijini Lilongwe.

Wekundu hao wanarejea nchini humo wakiwa na kumbukumbu nzuri waliposhinda mabao 2-0 mbele ya Nyasa Big Bullet, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Septemba 10, 2022 Uwanja wa Bingu, kwa mabao ya Moses Phili yaliyosha kuipa heshima Simba ugenini.

Simba imeanza msimu huu 2026-2027 kwa kasi ikishinda mechi nne mfululizo za Ligi Kuu, hali ambayo imeonekana kuwapa mzuka mashabiki katika kufanya vizuri kwenye mashindano yake.

Katika mechi hizo, Simba imeshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, ikaichapa Pamba Jiji 2-1 sawa na ushindi dhidi ya Singida Black Stars 2-1 na ikainyuka Coastal Union bao 1-0 na kuvuna pointi 12 ikikaa kileleni kwenye msimamo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba Mkoa wa Mbeya, Yusuph Mwandete, amesema mwanzo mzuri wa timu msimu huu na malengo waliyotangaza uongozi wa juu, hawana sababu ya kutoa sapoti ili kufikia ndoto zao.

Amesema katika kuunga mkono juhudi, Simba mkoani Mbeya wameandaa usafiri wa mabasi matano yenye kubeba abiria 30 kila moja, sawa na mashabiki 150 ambao watatua jiji la Lilongwe kuipa nguvu timu hiyo.

“Hatuendi kwa historia kwakuwa mpira ni mchezo wa wazi, lakini kwa uwezo na ubora wa kikosi chetu pamoja na mipango ya timu kwa ujumla tunaona msimu huu ni wetu kuanzia Ligi Kuu hadi kimataifa.

“Mashabiki tumehamasika tumekubali kujichanga kwenda Malawi kuisapoti timu, tunatarajia kuwa na coaster tano kila moja inabeba abiria 30, hivyo tunaamini tutashinda na kuanza mapema kampeni kuisaka fainali klabu bingwa mwaka huu,” amesema Mwandete.

Kwa upande wake, Benjamin James, amesema msimu huu Simba haina staa mmoja, bali kikosi chote kimesheheni nyota ambao yeyote anaweza kuamua mechi akiomba mashabiki wote nchini kuifuata timu Malawi.

“Twende tukavamie kwa nguvu zetu kama tulivyofanya kipindi kile, kimsingi kocha asiwabeze wapinzani, twende kwa nidhamu na heshima kwakuwa wapinzani ni bingwa Ligi Kuu huko kwao,” amesema James.

Baada ya mchezo huo wa ugenini, Simba itarejea nyumbani kuikaribisha Mighty Wanderers Septemba 11, 2026 ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya pili kwa kucheza na mshindi kati ya 15 De Agosto na Fomboni kuwania kucheza makundi.