Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Filex afichua alivyokosa dili Polisi Tanzania

FELIX Pict

ALIYEKUWA beki wa Fufuni, Filex Bryson, ametaja sababu iliyokwamisha kujiunga na Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, beki huyo amesema Polisi Tanzania ilimtaka asajiliwe timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 20, jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Amesema, mkataba huo kwake aliona haukuwa mzuri kwa sababu alihitaji kucheza timu ya wakubwa na si vijana licha ya kufaulu majaribio aliyofanya.

“Viongozi wa timu hiyo walitaka nisaini mkataba timu ya vijana, kwa upande wangu nikaona si sahihi japokuwa nilifaulu majaribio,” amesema.

Filex amesema baada ya kuona hali hiyo, ndipo alipoamua kurudi Dar es Salaam kuangalia upande mwingine huku akisubiria dirisha dogo.

Amesema, kwasasa hana timu yoyote kwani ni mchezaji huru, hivyo anapambana kulinda kipaji chake na kuangalia fursa nyingine kipindi cha dirisha dogo.