Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fagio la chuma kupita Napoli

Muktasari:

Hii hapa orodha ya mastaa watano wanaoweza kuuzwa Napoli na timu zinazotajwa kwamba huenda wakaenda kujiunga nazo.

NAPLES, ITALIA . HUKO Napoli mambo si mambo, ndani na nje ya uwanja. Baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya Genoa, Jumamosi iliyopita, kikosi hicho cha Kocha Carlo Ancelotti sasa kinashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Serie A, pointi tano nyuma ya nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na pointi 13 nyuma ya vinara Juventus.

Hata hivyo, hilo la matokeo halionekani kuwa shida kubwa zaidi ya lile la wachezaji kutibuana na mmiliki wa timu hiyo, Aurelio Di Laurentiis na kuna wachezaji watafunguliwa mlango wa kutokea katika dirisha lijalo la usajili.

Hii hapa orodha ya mastaa watano wanaoweza kuuzwa Napoli na timu zinazotajwa kwamba huenda wakaenda kujiunga nazo.

5. Dries Mertens (Inter)

Itakuwa majanga wakati Dries Mertens atakapoondoka Napoli. Staa huyu amekuwa na uhusiano mzuri na mashabiki wa timu hiyo huku akiweka rekodi zake sawa, akiwa kinara wa mabao wa muda wote kwenye kikosi hicho cha Napoli.

Hata hivyo, Mbelgiji huyo ni moja ya wachezaji wanaoweza kuuzwa mwisho wa msimu huku Inter wakitajwa kwenye uwezekano wa kunasa saini yake.

4.Kalidou Koulibaly (Man United)

Kama kuna mchezaji ambaye bila ya shaka ataachana na Napoli basi ni Kalidou Koulibaly.

Beki huyo wa kati amekuwa gumzo huko Ulaya, akisakwa na klabu mbalimbali wakiwamo Manchester United, huku ikielezwa kama atauzwa basi hakuna jambo litakaloshangaza wengi kama ataonekana kwenye uzi wa Old Trafford kuanzia mwakani.

3.Fabian Ruiz (Real Madrid)

Mwezi uliopita, mawakala wa Real Madrid walifanya mawasiliano na Fabian Ruiz ili kumnasa staa huyo akakipige kwao Hispania.

Kinachotokea kwa sasa kwenye kikosi cha Napoli, Los Blancos watakuwa na nafasi kubwa ya kunasa saini ya mchezaji huyo kutokana na Napoli kwamba kuwa tayari kumuuza.

Barcelona na Manchester City nazo zimekuwa zikimfukuzia kiungo huyo.

2.Jose Callejon (Milan)

Wakati Ligi Kuu China ikionekana kama mwafaka kwa Callejon, mwandishi wa habari Mtaliano, Ciro Venerato amefichua AC Milan wamekuwa wakifukuzia saini ya Mhispaniola huyo ili kumnasa dili lake litakapofika tamati mwisho wa msimu huu huko Napoli.

Milan wao wanahitaji sana saini yake na kwamba wanafuatilia kinachoendelea huko Naples ili kumbeba jumla.

Lorenzo Insigne (Chelsea)

Marufuku ya kusajili ndicho kitu kinachotajwa kuwatibulia Chelsea kwenye mpango wao wa kumnasa staa Insigne.

Hata hivyo, sasa The Blues wamekata rufaa na kama wataruhusiwa kusajili Januari, bila ya shaka watakwenda kutua kwa staa huyo kwa sababu wanamtazama kama mrithi sahihi wa Eden Hazard.

Rufaa ikishindikana, basi mchakato wa kumnasa utakuwa wa mwisho wa msimu.