Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Waarabu kuikomoa Simba

Muktasari:

  • WAARABU wamechukizwa na kipigo. Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone dhidi ya Al Ahly linaelezwa kwamba limewafanya mabosi wa klabu hiyo ya Misri kutaka kumng’oa Konde Boy.

WAARABU wamechukizwa na kipigo. Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone dhidi ya Al Ahly linaelezwa kwamba limewafanya mabosi wa klabu hiyo ya Misri kutaka kumng’oa Konde Boy.

Luis alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wao wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwafanya Simba waongoze kundi A ikiwa na pointi sita.

Hii inakuwa sio kwa mara ya kwanza mchezaji huyu kuhitajika na klabu mbalimbali, lakini mabosi wa Simba wamekuwa wagumu kumuachia.

Pia inaelezwa ugumu wa mkataba wake unachangia mchezaji huyo kutoondoka kwani wakati anasajilkwa akitokea Ud Songo alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu Msimbazi.