Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dalali amsaka Mzee Mpili

MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ni kama ametupa jiwe gizani kwenda kwa Mzee Mpili baada ya timu yake kunyakua taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kwamba raha yao ni kuchukua vikombe vinavyotambulika na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na sio kupania mechi moja.

Dalali alisema hii ni mara nne mfululizo kutwaa Ligi Kuu Bara na ya pili kuchukua ASFC na yote yanatambulika na Caf na sio mbwembwe za Mzee Mpili kutambia mechi moja ambayo hawajaambulia kitu zaidi ya kujifariji.

Alisema alimtafuta Mzee Mpili baada ya fainali kuamua Simba bingwa hakumuona na wala hakuzisikia mbwembwe zake kama walivyocheza nao mechi ya mzunguko wa pili.

“Nilianza kumtafuta kabla ya mechi kuanza kutaka kumuuliza mzee mwenzangu vipi mbona una kimya kingi, lakini naona atakuwa ameishaelewa Simba ni levo nyingine, haina maneno zaidi ya kuonyesha shoo za kibabe,” alisema.

Alisema wakati Simba imepoteza mechi ya mzunguko wa pili wa ligi dhidi ya Yanga, Mzee Mpili alitamba kama vile alicheza namba yoyote uwanjani, jambo ambalo lilimshangaza na kutamba kwamba kazi yao ni kukusanya mataji.

“Simba ni levo nyingine, inatumia nguvu kubwa kuhakikisha inaandika historia ya kuchukua mataji yanayotambulika na Caf ili kwenda kukutana na mabingwa wengine Afrika, ndio maana na watani wetu wa jadi Yanga watacheza mwaka huu kupitia mgongo wa Simba,” alisema.

“Simba katika matokeo yote waliyoyapata msimu ulioisha iwe kwenye ligi ama ASFC imecheza mpira wa maana, ukiachana na hilo ndio maana ilifika robo fainali michuano ya Caf, tafsiri yake ni kwamba ina kikosi imara.”