Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dalali afunguka kilichompeleka Simba

MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali amefunguka juu ya uamuzi wake wa kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Swedy Mkwabi.

Mkwabi alijiuzulu nafasi hiyo Septemba mwaka jana ambapo ilikaimiwa na Mwina Kaduguda aliyepitishwa na mkutano mkuu uliofanyika Desemba mwaka jana.

Mkwabi aling’atuka madarakani akiwa ameitumikia Simba kwa mwaka mmoja pekee kwani alichaguliwa Novemba, 2018 na kwa mujibu wa Katiba ya Simba viongozi wa kuchaguliwa na wanachama hukaa miaka minne madarakani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dalali alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kufuatwa na wanachama ambao walitumia muda mwingi kumbembeleza ili achukuwe fomu hiyo aliyoichukuwa juzi Jumamosi.

Alisema mbali na kuombwa na wanachama wa Simba, lakini ni haki ya kila mwanachama kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi ili mradi awe na sifa zilizoorodheshwa ambapo yeye sifa hizo anazo.

“Ni haki ya mtu yeyote kuchukua fomu ya kugombea nafasi ndani ya Simba ili mradi tu ana vigezo na hakiuki Katiba, nimechukuwa fomu kwa kufuata kanuni za uchaguzi hivyo sipo nje ya kanuni hizo.

“Nilikuwa nakataa kuchukua hii fomu, imechukua muda mrefu kutafakari na kukubali maombi ya wanachama waliokuja nyumbani kwangu kuniomba nigombee, hivyo niliona acha nichukuwe,” alisema Dalali

Kiongozi huyo mkongwe alisema kwa sasa atasubiri taratibu zingine zilizowekwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti Boniface Lihamwike.