Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga wanapiga nyumbani ugenini

LIGI Kuu Tanzania Bara inazidi kushika kasi huku kila timu ikiendelea kutafuta pointi katika kutimiza malengo yake ya msimu kwa kumaliza nafasi sahihi na wengine wakiutafuta ubingwa.

Ushindani huo umekuwa ukizipa hrshima timu zingine zikiwa na makali sio tu nyumbani bali hata ugenini zimekuwa zikivuna pointi tatu na hapa tunaangalia timu ambazo zimevuna pointi nyingi ugenini kwa ushindi.


Yanga pointi 18 ugenini

Vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga acha wang’ae kutokana mpaka sasa ndio timu pekee iliyoshinda mechi nyingi ugenini kuliko hata kushinda nyumbani wakipata ushindi katika mechi 6.

Yanga imezichapa ugenini Kagera Sugar, KMC, Biashara, Azam, Mwadui, Mtibwa Sugar zikiwa katika viwanja vyao na kujihakikishia jumla ya pointi 18 huku nyumbani wakishinda mechi 6 dhidi ya Mbeya City, Coastal Union, Polisi Tanzania, JKT Tanzania,Ruvu Shooting na Dodoma Jiji.


Simba pointi 12

Simba wanafuata nyuma ya Yanga kama ambavyo ipo katika msimamo wa ligi na wao wakishinda katika mechi 4 za ugenini msimu huu ingawa wana viporo vyao ambavyo mpaka sasa havijaonyesha dalili ya kuchacha.

Simba imezifunga ugenini Ihefu ukia ndio mchezo wao wa kwanza katika ligi, kisha akavuna pointi tatu zingine kutoka kwa JKT Tanzania, Coastal Union na Mbeya City lakini pia wakalingana na Yanga kushinda nyumbani kila moja wakishinda mechi 6 wao wakizifunga Biashara United, Gwambina, Mwadui, Kagera Sugar, Polisi na KMC.


Azam, Polisi pointi 9

Azam ambao bado wanaumizwa na sare za mfululizo wamefungana na Polisi Tanzania katika kushika nafasi ya tatu kwenye timu zilizovuna pointi za ushindi ugenini kila moja ikivuna pointi 9.

Azam yenyewe imezifunga Mbeya City, Prisons, Ihefu katika mechi za mwanzo wa ligi wakiwa na kasi kubwa kiasi cha kuongoza ligi lakini wakati huo pia ilikuwa moto nyumbani ikishinda mechi 5 dhidi ya Polisi, Coastal Union, Kagera Sugar, Dodoma na Mwadui. Polisi nao wakavuna pointi 9 ugenini dhidi ya Namungo, KMC na Prisons huku wakiwa hoi nyumbani wakishinda mbili pekee dhidi ya Dodoma na Mtibwa Sugar.


Ruvu, KMC, Gwambina, Mbeya, JKT nao wamo

Timu tano zimekabana koo katika nafasi ya nne katika timu zilizoshinda ugenini kila moja ikivuna pointi sita ugenini katika mechi zao lakini wakatofautina zile za nyumbani.

Ruvu Shooting imevuna pointi sita ugenini dhidi ya klabu za JKT Tanzania na Simba lakini pia ikashinda mechi nne nyumbani dhidi ya Gwambina, Coastal Union, Mbeya City na Prisons.

KMC nao wamechukua pointi 6 ugenini kutoka kwa Mwadui na Gwambina lakini nyumbani wakachukua pointi nyingi zaidi wakishinda mechi nne dhidi ya Mbeya City, Prisons, Azam na baadaye Dodoma.

Gwambina nao wakachukua pointi sita ugenini dhidi ya JKT Tanzania na baadaye Mwadui kisha wakashinda mechi mbili nyumbani dhidi ya Ihefu na Mtibwa Sugar.

JKT Tanzania nao wakashinda mbili ugenini na kuwafanya kuvuna pointi sita dhidi ya Kagera Sugar kisha Mwadui lakini nyumbani wameshinda mchezo mmoja pekee dhidi ya Biashara.

Mbeya City takwimu zao zinashtua jamaa wameshinda mechi mbili ugenini dhidi ya Kagera Sugar na JKT Tanzania lakini ajabu hawajashinda mechi yoyote nyumbani msimu huu.

Biashara, Prisons, Dodoma, Mtibwa, Kagera, Coastal, Namungo, Mwadui nao angalau 3

Zipo timu nane ambazo nazo zimefungana zikiambulia pointi tatu ugenini lakini wakatofautiana katika zile walizoshinda nyumbani.

Biashara wameshinda mechi moja ugenini dhidi ya Polisi Tanzania lakini nyumbani kwao wamekuwa moto wakashinda mechi tano dhidi ya Gwambina, Mwadui, Mtibwa Sugar, Ihefu na Mbeya City. Prisons nao wameshinda moja tu ugenini dhidi ya Dodoma lakini nyumbani wakashinda mechi nne wakizifunga Namungo, bingwa mtetezi Simba, Ihefu na Mwadui.

Dodoma nao ugenini wameshinda mchezo mmoja pekee dhidi ya JKT Tanzania lakini nyumbani wakashinda michezo minne dhidi ya Mwadui, Ruvu Shooting, Ihefu na Gwambina.

Mtibwa nao wako katika kundi hilo wakishinda ugenini mechi moja dhidi ya Ihefu lakini nyumbani wakishinda mechi tano dhidi ya Namungo, Azam, Mwadui,KMC na juzi wakiifunga JKT Tanzania.

Kagera Sugar wamevuna pointi tatu tu ugenini dhidi Prisons lakini nyumbani wakashinda mechi tano dhidi ya KMC, Mtibwa Sugar, Mwadui, Biashara na Coastal Union.

Coastal Union nao wamemchapa Mtibwa Sugar pekee wakiwa ugenini na nyumbani wakashinda michezo mitatu mpaka sasa dhidi ya JKT Tanzania, Biashara United na Ihefu walipotembelea uwanja wao wa Mkwakwani.

Namungo ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho waliosalia nao wameshinda ugenini mchezo mmoja pekee dhidi ya Mbeya City lakini nyumbani wakashinda mechi tatu dhidi ya Coastal Union, Kagera Sugar na Dodoma.

Mwadui ambao ndio timu iliyofungwa mabao mengi msimu huu mpaka sasa wao nao wameambulia pointi tatu ugenini alipowachapa wenyeji wao Namungo na nyumbani kwao wameshinda mechi mbili pekee dhidi ya Ihefu na Mbeya City.


Ihefu yajikongoja

Ihefu ambao wamepanda ligi msimu huu angalau sasa nao wanajikongoja,jamaa mpaka sasa hawaujui utamu wa ushindi wa ugenini baada ya kushindwa kushinda mechi yoyote ugenini lakini nyumbani pia hali yao ilikuwa sio nzuri, japo kwa sasa wanapumua. Wageni ho nao wamefufuka kwa kushinda mechi tatu za nyumbani zikiwa mbili mfululizo walizoshinda hivi kribuni dhidi ya Kagera Sugar na KMC na sare dhidi ya JKT Tanzania.