Chirwa: Ubingwa lazima, Biashara tunawapiga
Muktasari:
STRAIKA wa Azam FC, Obrey Chirwa amewahakikishia viongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa mechi yao ya kesho Jumatatu dhidi ya Biashara United lazima washinde na ubingwa utatua Chamazi.
MWANDISHI WETU
STRAIKA wa Azam FC, Obrey Chirwa amewahakikishia viongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa mechi yao ya kesho Jumatatu dhidi ya Biashara United lazima washinde na ubingwa utatua Chamazi.
Azam ipo ugenini kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma huku timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kichapo kwenye michezo yao iliyopita.
Wenyeji Biashara wametoka kufungwa bao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar huku Azam wao walipoteza dhidi ya Yanga bao 1-0 wakiwa nyumbani Uwanja wa Azam Complex na kupelekea kocha Aristico Cioaba wao kufutwa kazi.
Azam ilianza ligi vizuri lakini baadaye hawakupata matokeo mazuri ambapo sasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 25 ikitanguliwa na Yanga wenye pointi 31 sasa wakati Biashara wanashika nafasi ya saba wakikusanya pointi 18.
Chirwa amesema pamoja na kwamba timu yao haijawahi kupata matokeo mazuri kwenye uwanja huo lakini nia yao sasa itatimia ya kuvuna pointi tatu.
"Tutafanya vizuri hii mechi, malengo yetu ni ubingwa, naamini tutarudi kwenye kiwango chetu cha mwanzo, lazima tujipange upya maana haiwezekani kuendelea kupoteza mechi mfululizo,"