Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chino Wana Man ateka mashabiki Uwanja wa Uhuru

Muktasari:

  • Chino anayeimba nyimbo za amapiano, aliingia Uwanja wa Uhuru akiwa juu ya moja ya magari matatu, yaliyoingia huku akiamsha shangwe kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

MSANII wa kizazi kipya, Chino Kidd 'Chino Wana Man', ameteka mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Uhuru, wakati wa kilele cha tamasha la Simba Day, linalofanyika leo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 90 ya klabu hiyo tangu kuanzishwa mwaka 1936.

Chino anayeimba nyimbo za amapiano, aliingia Uwanja wa Uhuru akiwa juu ya moja ya magari matatu, yaliyoingia huku akiamsha shangwe kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

Msanii huyo aliingia na msafara wa magari matatu yakiwa yamezungukwa na ulinzi mkali, ambapo alianza kuimba nyimbo mbalimbali zikiwemo fashion na tunakuja kama mazombi, jambo lililoibuka shangwe uwanjani hapo.

Hata hivyo, baada ya shangwe kubwa la mashabiki, msanii huyo alishuka chini ya gari na kuanza kuimba kwa kuzunguka uwanja na kuamsha hisia zaidi kutokana kupokelewa vizuri.

Hatua hiyo ya msainii huyo kushuka chini, iliamsha baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani ili kuungana naye kuimba, japo maofisa wa usalama waliokuwa wanamlimda walihakikisha anafanya kazi yake vizuri bila ya shida yoyote.