Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chilambo achiwa msala wa Kapombe

CHILAMBO Pict

Muktasari:

  • Kapombe ambaye ni nahodha wa Simba, alipata majeraha ya mkono katika mashindano ya CECAFA Kagame yaliyofanyika Kigali, Rwanda, baada ya kugongana na kipa Hussein Abel katika mchezo wa michuano hiyo.

KOCHA wa Simba, Steve Barker amewashusha presha Wanasimba kufuatia kukosa huduma ya wachezaji wake wawili, Shomary Kapombe na David Kameta ‘Duchu’, ambao wote wamekuwa wakitumika katika nafasi ya beki ya kulia.

Kapombe ambaye ni nahodha wa Simba, alipata majeraha ya mkono katika mashindano ya CECAFA Kagame yaliyofanyika Kigali, Rwanda, baada ya kugongana na kipa Hussein Abel katika mchezo wa michuano hiyo.

Huku kwa upande wa Duchu, beki huyo alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa Simba wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar baada ya kumchezea vibaya David Luhende.

Kutokana na kadi hiyo nyekundu, Duchu atakosa mchezo wa leo dhidi ya Pamba Jiji utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, hali iliyomlazimisha Barker kufanya mabadiliko katika eneo hilo.

Barker amesema majeraha na adhabu za wachezaji ni sehemu ya changamoto ambazo timu hukutana nazo katika msimu, hivyo Simba imejiandaa kukabiliana nazo bila kuathiri malengo yake.

“Hivi ni vitu ambavyo hutokea katika msimu, mchezaji anaweza kuumia au kupata adhabu, lakini kama timu lazima iwe tayari kukabiliana na hali hiyo,” amesema Barker.

Kocha huyo amesema muhimu ni kuwa na kikosi chenye wachezaji wengi wenye uwezo ili pindi mmoja anapokosekana, mwingine awe tayari kuchukua nafasi yake na kuendeleza ushindani.

Kutokuwepo kwa Kapombe na Duchu kumetoa nafasi kwa Nathaniel Chilambo kuanza kuonyesha uwezo wake ndani ya kikosi cha Simba huku akitarajiwa kuanza katika mchezo huo dhidi ya Pamba Jiji.

Chilambo alijiunga na Simba akitokea Azam FC katika dirisha hili la usajili na mchezo wa leo unaweza kuwa mwanzo wake rasmi wa kuanza kuandika historia yake ndani ya kikosi hicho.