Carlinhos, Fiston wapewa rungu Yanga

KOCHA Cedric Kaze hataki tena kukatwa stimu na mashabiki na amepania kesho kuliingiza jeshi lake likiwa na sura nyingine kwa kuamua kuwaanzisha kwa pamoja, Fiston Abdulrazack na Carlinhos, huku Yacouba Songne akitarajiwa kurejea uwanjani baada ya kukosekana muda mrefu.

Kuna uwezekano mkubwa kocha huyo akabadilisha jeshi lake litakapovaana na Ken Gold (zamani Gipco) katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (ASFC) kesho Jumamosi, huku akiwapigisha tizi vijana wake kama wanaenda kucheza mechi ya fainali kuonyesha hataki tena lawama na mtu.

Soma zaidi hapa: www.egazeti.co.tz