Caf yalegeza kanunia za Corona

Friday January 15 2021
New Content Item (1)
By Mwandishi Wetu

YAOUNDE, CAMEROON. IKIWA ni siku chache tangu shirikisho la soka barani Afrika barani (CAF) litangaze kwamba timu yoyote  itakayokuwa haina wachezaji 11 akiwemo golikipa sambamba na wachezaji wanne wa akiba kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya Corona haitaruhusiwa kucheza mechi zilizo chini ya shirikisho hilo na itahesabika imepoteza mchezo husika kwa mabao 2-0.

Taarifa mpya imetolewa baada ya kikao cha kamati ya Utendaji kilichokaliwa leo Januari 15, huko Jijini Yaounde nchini Cameroon.

Kamati hiyo ilipitia tena taarifa yake iliyotoa Januari 8 na kuifanyia maboresho yaliyokuja na ripoti mpya inayoeleza, kama timu haina wachezaji wanne wa akiba na wachezaji 11 akiwemo na golikipa itaruhusiwa kucheza mechi.

"Tunaruhusu timu yenye wachezaji 11 kucheza mechi husika na kama kwenye wachezaji hao 11 hakutakuwa na golikipa, mchezaji yeyote anaweza akadaka,"

Taarifa hiyo inafafanua, sharti la kwanza timu kuruhusiwa kucheza mchezo ulio chini ya shirikisho ni kuwa na wachezaji wasiopungua 11 wasiokuwa na maambukizi ya virusi vya Corona bila ya kujali uwepo wa golikipa na kama timu haitakuwa na wachezaji 11 haitaruhusiwa kucheza na itakuwa imepoteza mchezo husika kwa kipigo cha mabao 2-0.

Aidha Caf ilisisitiza, mchezaji yoyote ambaye atakutwa na maambukizi ya Corona hataruhusiwa kucheza mechi husika.

Advertisement
Advertisement