Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco, Kagere wamaliza utata

Bocco, Kagere wamaliza utata

NAHODHA wa Simba, John Bocco 'Adebayor' amesema hana tatizo lolote na mshambuliaji mwenzake Meddie Kagere 'MK 14' baada ya kuibuka mjadala mtandaoni kuhusu tukio la ushangiliaji wa bao la kwanza dakika ya 64 liliofungwa na Clatous Chama 'Triple C'.

Baada ya Chama kufunga bao hilo alienda pembeni mwa lango kushangilia na Bocco, kisha Kagere alifuatia japo Bocco aliwahi kuondoka bila mkono wa Kagere aliomuelekezea kumgusa.

Mitandao ya kijamii hususani Instagram na WhatsApp ilitembea video hiyo na kuibua mijadala ambayo Bocco aliizima kwa kujibu kuwa hakuna tatizo lolote.

Licha ya kujibu mmoja mmoja, Bocco ameamua kuandika kwenye akaunti yake ya Instagram akisisitiza hana tatizo na Kagere bali watu wametafsiri kitendo hicho kwa mihemko.

“Hatuna tofauti yoyote na Medi tupo sawa... walicho kitafsiri watu ni mihemko yao ya kilasiku yakukosa habari na kutaka kutengeneza story zisizo na kichwa wala miguu. Sina shida na Medi na wala medi hana shida na mimi pia timu yetu hatuna tatizo lolote ni amani na upendo hizo zilikua fikra na hisia za watu kutafsiri na kuhisi vitu visivo kuwa na uhalisia na uwakika,” ameandika Bocco

Kwa upande wake Kagere amesema hajawahi kuwa na mgogoro au tatizo na nahodha wake huyo au mchezaji yeyote wa Simba.

“Napenda kuwa muwazi kwenye juu ya hili suala langu na Bocco, sijawahi kuwa na mgogoro au tatizo nae au mchezaji yeyote Simba. Binafsi napenda tupambanae na adui zetu kuliko sisi wenyewe. Naimani mmeelewa” ameandika Kagere

Nyota hao wawili ambao wanacheza pamoja kwa msimu wa tatu mfululizo wamehusika kutengeneza jumla ya mabao 81, Bocco ambaye ndiye kinara wa mabao kwa sasa katika ligi ya msimu huu akifunga 32 na Kagere aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya akiwa na 49.

Kwa msimu huu Kagere ambaye ametwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa misimu miwili iliyopita, ameshafunga mabao manne, ikiwa ni matatu pungufu na aliyonayo Bocco mwenye saba akiongoza orodha.

Mwandishi Wetu