Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Orlando kuikosa Simba

Beki Orlando Kuikosa Simba

Muktasari:

  • Mako alikuwa amepoteza fahamu na alipatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa kabla ya kuondolewa uwanjani kwa gari la wagonjwa na kupelekwa hospitalini.

Beki wa kushoto wa Orlando Pirates Paseka Mako aliondolewa uwanjani hapo jana kwa gari la wagonjwa baada ya kuumia katika mechi ya DStv Premiership dhidi ya Baroka FC kwenye Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane.

Mako alikuwa amepoteza fahamu na alipatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa kabla ya kuondolewa uwanjani kwa gari la wagonjwa na kupelekwa hospitalini.

Taarifa kutoka Pirates zinasema “Kufuatia jeraha la dharura lililomhusisha beki Paseka Mako kwenye mechi ya DStv Premiership dhidi ya Baroka FC jana usiku, Klabu ya Orlando Pirates inaweza kuthibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yuko katika hali nzuri.

"Daktari amefichua kuwa matokeo ya uchunguzi wa CAT hayajaonyesha dalili za kuvunjika kwa fuvu la kichwa au kuvuja damu kwenye ubongo. Hata hivyo, mchezaji huyo amepata jeraha kwenye uso na pua.

Orlando wanatarajia kucheza mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba Aprili 17 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.