Balama: Mukoko anajua sana
BAADA ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, kiungo wa Yanga, Balama Mapinduzi amemtaja Mukoko Tonombe kumvutia ndani ya kikosi hicho kwa namna anavyowajibika kusaidiana na mabeki kuhakikisha ukuta wao unakuwa salama.
Majeraha ya kisigino yanamuweka nje Balama tangu alivyoumia msimu wa 2019/20 kwenye mazoezi ya kujiandaa dhidi ya Ndanda FC kabla haijashuka daraja.
Balama alisema japo yupo nje ya uwanja, lakini hajaacha kuifuatilia Ligi Kuu na timu yake inavyocheza ndiyo maana imekuwa rahisi kujua anachofanya Mukoko.
“Kuna wachezaji hawazungumzwi sana, lakini uwanjani wana kazi kubwa na ngumu wanayoifanya, kwa upande wangu ukiniambia nikutajie mchezaji bora wa ligi msimu huu, basi Mukoko nampa nafasi kubwa, amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu na ni bora,” alisema.