Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF yapewa darasa la soka ajira

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa Agosti 8, 2026 na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, katika hafla ya tuzo za ZFF msimu wa nne iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Amaan Complex, Zanzibar.

LICHA ya Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Zanzibar (ZFF) na Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar (ZBL) kupewa pongezi kwa utendaji kazi, pia wametakiwa kukaa pamoja na klabu kuzifahamisha umuhimu wa kuwa na mpira wenye nidhamu na viwango kuelekea katika soka la ajira.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 8, 2026 na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, katika hafla ya tuzo za ZFF msimu wa nne iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Amaan Complex, Zanzibar.

Alisema, ili kupata wadhamini wa Ligi Kuu Zanzibar, ZFF wanapaswa kuangalia upungufu uliopo katika soka la Zanzibar kwa klabu, waamuzi, wakufunzi na wachezaji kisheria na kikanuni.

Alisema, wakibaini upungufu uliopo na kufanyia kazi, watachukua hatua stahiki za kukemea uharibifu wa miundombinu ya michezo na ligi kwa jumla.

“Naipongeza Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar kwa kushirikiana na ZFF, nawataka mkae pamoja na klabu kuzifahamisha umuhimu wa kuwa na mpira wenye viwango na nidhamu ili kuelekea mpira wa ajira tunaoutaka,” alisema Abdulla.

Alisema shirikisho hilo limepata mafanikio katika kuboresha utawala wa michezo, kuimarisha mashindano ya ndani pamoja na kuanzisha mifumo ya kisasa ya kidijitali inayoongoza uwazi na ufanisi katika usimamizi wa mpira.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa ZFF, Yahya Abdalla Shamuni, alisema Shirikisho hilo limefanya mageuzi katika usimamizi wa mpira wenye lengo la kuendana na mabadiliko ya soka duniani.

Aidha, ameiomba Serikali kuwasaidia kupata wadhamini wengi zaidi watakaodhamini Ligi Kuu ya Soka Zanzibar na kuifanya kuwa na ushindani.

Akizungumza kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, alisema mashirikisho hayo yanafanyakazi kwa karibu kuangalia maslahi na changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.

Cornel amewakumbusha viongozi, wakufunzi, klabu, wachezaji na wadau wa soka Tanzania kuheshimu na kufuata kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu ili kuimarika zaidi.