Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kangwada ameshachanga vyema karata

KANGWANDA Pict

Muktasari:

  • Hizi timu zetu bhana tunazifahamu jinsi ambavyo zinaipa uzito mkubwa mechi baina yao, hivyo unaweza kuamua hatima ya mchezaji kwenye timu awe na maisha marefu au akae kwa muda mfupi.

KWA kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii juzi Jumatano, yule Albert Kangwanda amejitengenezea mazingira mazuri ya kula maisha pale Yanga.

Hizi timu zetu bhana tunazifahamu jinsi ambavyo zinaipa uzito mkubwa mechi baina yao, hivyo unaweza kuamua hatima ya mchezaji kwenye timu awe na maisha marefu au akae kwa muda mfupi.

Kijiwe kina kumbukumbu ya jinsi baadhi ya wachezaji walimvyobebwa na kufanya kwao vizuri katika mechi ya watani na wale ambao mambo kwao yalikuwa magumu baada ya kuchemsha katika Dabi ya Kariakoo.

Mfano wa wachezaji ambao maisha yao yalikuwa matamu katika klabu hizo kisa kufanya mabalaa katika Kariakoo Dabi ni Musa Mgosi, Jerry Tegete, Mrisho Ngassa, Emmanuel Okwi, Ben Mwalala na Dua Said.

Lakini wapo ambao mechi baina ya timu hizo iliwaletea nuksi baada ya kutofanya vizuri kama vile Chibe Chibindu, Hussein Kazi, Benito John, Kelvin Kijili, Hassan Kessy na Ally Mustapha ‘Barthez’.

Ni rahisi kwa hizi timu mbili kumvumilia mchezaji ambaye haonyeshi kiwango kizuri kwa muendelezo, kwa sababu tu aliwasha moto dhidi ya mtani kwa kufunga bao, kusababisha penalti na hata kupiga pasi ya mwisho.

Sasa kwa Kangwanda bao lake limekuja muda sahihi kwa vile yeye ni mgeni hivyo ataanza akiwa hana presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga tofauti na iwapo asingefanya vizuri juzi.

Pia inamtengenezea mazingira mazuri ya kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga kwa vile mchezo dhidi ya Simba ndio kipimo kikubwa cha ufanisi wa mchezaji.

Kangwanda ameanza kwa kufaulu mtihani wake wa kwanza, kazi kwake sasa kulinda nafasi yake kikosini.