Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho majanga, nje wiki tatu

YANGA inajiandaa kushuka uwanjani jioni hii kuvaana na Namungo katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, mjini Lindi huku ikiwakosa nyota wake sita akiwamo Kiungo Khalid Aucho ambaye imefahamika atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu kutokana na kufanyiwa upasuaji wa goti.

Wengine wanaoikosa mechi hiyo ya leo ni kipa Djigui Diarra, beki Joyce Lomalisa, kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua na washambuliaji Joseph Guede na Kennedy Musonda, huku Aucho aliyeumia katika mechi ya mwisho ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri iliyoshinda bao 1-0 jijini Cairo atazikosa nyingine tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa timu yake, imethibitishwa Aucho kufanyiwa upasuaji huo.

"Tutamkosa Daktari wa Mpira (jina utani la Aucho) kwa wiki tatu kutokana na upasuaji aliofanyiwa hivyo mashabiki na wanachama wa timu yetu tunaomba mumuombee mchezaji wetu aweze kurudi kwenye majukumu yake mapema," imesomeka taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu hiyo ya Yanga iliyongeza kuwa;

"Upasuaji umekwenda vizuri na mchezaji wetu yupo kwenye hali nzuri kinachotakiwa sasa ni kupata mapumziko kwa muda aliopewa ili aweze kurudi akiwa katika hali nzuri na ya ushindani."
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amethibitisha ni kweli mchezaji huyo amefanyiwa upasuaji baada ya kugundua tatizo hilo ambalo alilipata kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Amesema kwa mujibu wa taarifa za awali za daktari, mchezaji huyo atakuwa nje kwa wiki tatu akiuguza jeraha hilo, huku akikosa mechi tatu zijazo za Ligi Kuu kabla ya kusimama kupisha kalenda ya FIFA na mechi za kimataifa za timu za taifa. Mechi tatu zijazo za Yanga ni dhidi ya Ihefu FC iliyowafumua mabao 2-1 zilipokutana Highland Estate Mbarali jijini Mbeya, Geita Gold na Azam FC iliyopangwa kupigwa Machi 17.

Katika mechi za kwanza Geita ilifungwa mabao 3-0 na Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na iliipasua Azam mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Azam Complex na timu hiyo kabla ya mechi ya leo jioni ilikuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 nyuma ya Azam yenye 44.