Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AS Vita kuweka kambi siku 14 Dar

Kikosi cha AS Vita ya DR Congo kipo njiani kuja nchini Tanzania kuweka kambi ya siku 14 kujiandaa na msimu mpya.

Vita wakiwa hapa wanataka kuweka kambi yao jijini Dar es Salaam ikiwa ni ushauri wa kocha wao msaidizi Raul Shungu.

Shungu aliwahi kufanya kazi nchini miaka ya nyuma akiifundisha Yanga kwa mafanikio kwa kutwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kikosi hicho kinachofundishwa na kocha Mfaransa Dominique Cionci pia kimepanga kucheza mechi kadhaa za kirafiki hapa nchini.

Bado haijafahamika endapo kama kitacheza na miamba ya soka Tanzania Yanga, Simba au Azam katika ratiba yao hiyo.

"Tunakuja Tanzania tutaweka kambi hapo kujiandaa na msimu mpya, tumeona tuje Tanzania hasa hapo Dar es Salaam kuna viwanja vizuri,  tutaangalia kama tutapata kucheza mechi na timu za hapo hizi kubwa," amesema Shungu.