Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwasa ampa akili mpya Kibwana

MKWASA Pict

Muktasari:

  • Mkwasa amesema Yao amerejea akiwa katika kiwango kizuri na sasa ushindani wa nafasi hiyo unamlazimisha Kibwana kuongeza juhudi ili kumshawishi kocha kuwa anastahili kuanza.

KOCHA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Boniface Mkwasa, amesema beki wa kulia, Kibwana Shomari, anapaswa kuonyesha kazi ya ziada ili kupata nafasi kwenye kikosi cha Yanga kutokana na kiwango kikubwa kinachoonyeshwa na Kouassi Attohoula Yao tangu aliporejea baada ya kupona majeraha.

Mkwasa amesema Yao amerejea akiwa katika kiwango kizuri na sasa ushindani wa nafasi hiyo unamlazimisha Kibwana kuongeza juhudi ili kumshawishi kocha kuwa anastahili kuanza.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mkwasa amesema hakuna kocha anayependa kumuacha nje mchezaji mwenye uwezo, hivyo Kibwana anapaswa kuongeza juhudi na kupambana zaidi ili kushindania nafasi hiyo.

“Kwa kiwango ambacho Yao anaonyesha, Kibwana ana kazi kubwa ya kufanya ili kupata nafasi. Hakuna kocha anayetamani kuwa na mchezaji mwenye uwezo mdogo, kwa hiyo naamini Kibwana ana uwezo mkubwa, lakini anapaswa kupambana zaidi ya pale,” amesema Mkwasa.

MKWA 01

Kinachomfanya Yao kuonekana tofauti kwa sasa siyo tu namna anavyocheza wakati Yanga ikiwa na mpira, bali pia kasi yake ya kurejea wakati timu inapopoteza mpira.

Mkwasa amesema hilo ni jambo ambalo linapaswa kuwa mfano kwa wachezaji wengine wa Tanzania, hasa wale wanaorejea baada ya majeraha, kwa sababu Yao amefuata hatua zote alizopewa na benchi la ufundi.

Kwa mujibu wa Mkwasa, Yao hakurudi uwanjani moja kwa moja na kucheza dakika 90, bali alianza taratibu kwa kupewa dakika chache, akaongeza hadi kufikia muda ambao mwili wake ulikuwa tayari kucheza mechi nzima.

“Ukiangalia alichokifanya Yao, amefuata muongozo wa kocha. Alianza kwa dakika tano, akaenda 10, 30 na baadaye akafika dakika 90 alipokuwa tayari kabisa. Huyu ni mchezaji ambaye amefanya kila kitu alichoelekezwa hata alipokuwa kwenye kipindi kigumu,” amesema.

MKWA 02

Mkwasa amesema tofauti na baadhi ya wachezaji ambao wanapona majeraha na kutaka kurudi haraka kucheza muda wote, Yao amekuwa na subira na kufuata programu iliyowekwa na benchi la ufundi.

“Wachezaji wengi wetu hawafuati kile wanachopewa na makocha wanapotoka kwenye majeraha. Wanataka kurudi haraka, halafu mwisho wa siku wanapotea. Yao amefanya tofauti,” amesema Mkwasa.

Yao anaonekana kuwa sehemu muhimu ya namna Yanga inavyocheza, kwani anapanda wakati timu ikiwa kwenye mashambulizi na wakati mwingine anaingia katikati ya uwanja kusaidia kujenga mashambulizi.

MKWA 03

Mkwasa amesifu pia uwezo wake wa kubadilika kulingana na hali ya mchezo, akisema wakati Yanga inashambulia, Yao anaweza kuonekana akiwa juu kusaidia mashambulizi, lakini timu inapopoteza mpira anarudi kwa kasi kusaidia safu ya ulinzi.