Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

29 kuchuana Karume Cup Zanzibar

KARUME Pict

Muktasari:

  • Kwa unguja michuano hiyo inafanyika Uwanja wa Mao Zedong, timu 16 zitashiriki ambapo za wanaume ni 12 na nne wanawake.

TIMU 29 Zanzibar zinashiriki mashindano ya Karume Cup ya mpira wa kikapu, yaliyoanza jana Jumapili Agosti 30, 2026 katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa unguja michuano hiyo inafanyika Uwanja wa Mao Zedong, timu 16 zitashiriki ambapo za wanaume ni 12 na nne wanawake.

Timu za wanaume zimegawanywa katika makundi mawili, ambapo Kundi A lina Miembeni, Polisi, Zimamoto, African Magic, Vetras na New West. Kwa upande wa Kundi B, linaundwa na Stone Town, JKU, Nyuki, Mpendae, Cavaliers na Mbuyuni, huku wanawake, timu nne zitakazoshiriki ni KVZ, JKU, Mafunzo na Mchina Queens.

Katibu wa Kamati ya Mashindano na Ufundi, Said Ali Mansab, amesema kwa upande wa Pemba, itawakilishwa na timu 13 zikiwemo tisa za wanaume na nne za wanawake.

Alizitaja timu za wanaume ni Clickers, Mkoani Bulls, Kangani, Tornado, Kichungwani, California, Dolphin, Sweet Bulls na Magangasi, huku wanawake ni PBC Queens, Chake Star, Wete Star na Micheweni Stars.

Awali, Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Zanzibar (ZBF), Thani Lali Mfamau, amesema mashindano hayo msimu huu yatachezwa tofauti kwa kila upande kutoa mshindi wake, akifafanua kwamba mwaka jana timu zilizofanya vizuri Pemba zilikwenda Unguja kwa ajili ya hatua ya mwisho, lakini mwaka huu mashindano yamepangwa kufanyika katika mfumo wa kanda pekee. Amesema mfumo huo unalenga kuongeza ushindani katika kila kanda na kutoa nafasi kwa timu nyingi kushiriki katika mazingira yao kabla ya kukutana katika kiwango cha juu zaidi katika mashindano yajayo.

Aidha amesema kupitia mashindano hayo, timu zimeruhusiwa kuchukua wachezaji hata kutoka nje ya Zanzibar. Mashindano hayo ni ya timu za wakubwa, yakihusisha wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 18, huku mashindano maalumu kwa vijana walio chini ya miaka 18 yakitarajiwa kufanyika Oktoba au Novemba mwaka huu.