Yikpe wala hana presha

KAMA unadhani kelele zinazopigwa na mashabiki dhidi ya Yikpe Gnamien, zinampa presha straika huyo mwili jumba, basi umekosea jamaa anasema kelele hizo hazimsumbui kwa vile anaamini muda utaongea na kuwapa raha mashabiki wa Yanga.
Yikpe amekuwa akibezwa mara kwa mara na mashabiki wa Yanga, huku wengine wakisema avunjiwe mkataba, lakini akizungumza na Mwanaspoti mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast amesema mwanzoni maneno yalikuwa yanamsumbua lakini hivi sasa anayachukulia kawaida.
“Watu wanaongea sana, ila siwasikilizi, wanaweza kuongea ukifanya vibaya na wanaweza kuongea nikifanya vizuri, mimi ni mchezaji wa Yanga na nina mkataba nao, hivyo watu sahihi wa kuzungumzia hilo kama wananiacha ni viongozi na sijasikia lolote kwao,” alisema Yikpe aliyefunga bao moja tu mpaka sasa katika Ligi Kuu tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya.
Yikpe amesema kwa upande wake amekuwa akifanya mazoezi muda wote ambao Ligi ilisimama ana anachosubiri ni kupata nafasi.
“Suala la kupata nafasi ya kucheza lipo kwa kocha.”