Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratiba ya ligi ikiwa ileile, soka linaenda kuzimu

Muktasari:

Katika jambo ambalo mwandishi wa makala haya alikuwa akilipigia kelele kila kukicha ni mfumo wa ligi, jambo ambalo lilimweka mbali mno na utawala uliopita ambao ulimuona kama msaliti na kutompa nafasi yeyote ya kusogea katika taaluma yake na kuwaacha wadogo zake wakipaa kila kukicha.

SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF) kupitia kwa msemaji wake Boniface Wambura limesema ratiba ya ligi itatoka mwezi mmoja kabla ya Agosti 20, mwaka huu.

Ratiba hiyo itakuwa uwanjani na kila timu itajua inaanza wapi ili ijipange vizuri.

Uongozi uliopita uliokuwa chini ya Leodeger Chilla Tenga ulifanya mambo mengi mazuri ambayo kimsingi ni lazima yaigwe na kuenziwa na utawala wa sasa.

Uongozi huo uliweka utawala safi wa kujua nani anawajibika kwa hili na nani anawajibika kwa lile. Ilikuwa si rahisi kumshika ubaya Tenga kwa kuwa mambo yote aliyaacha kwa watendaji wake, wakati mwingine ni safi ingawaje wakati mwingine ni tatizo.

Katika jambo ambalo mwandishi wa makala haya alikuwa akilipigia kelele kila kukicha ni mfumo wa ligi, jambo ambalo lilimweka mbali mno na utawala uliopita ambao ulimuona kama msaliti na kutompa nafasi yeyote ya kusogea katika taaluma yake na kuwaacha wadogo zake wakipaa kila kukicha.

Katika mengi mazuri waliyoyafanya moja la mfumo wa ligi kwangu ilikuwa ni tatizo na naamini ndilo lililotufikisha hapa tulipo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa wakati ule aliua ligi zote za chini na kuanzisha ligi moja tu ya TFF, mfumo ambao sikuukubali hadi leo.

Mwaka 2007 ikachezwa ligi ndogo ya kubadili mfumo ili tuwaige Waingereza kuanza ligi Agosti na kumaliza Mei. Wote tulipongeza tukasubiri utekelezaji, hapo ndipo palipokuwa na kichekesho wenye kuona tukapiga kelele, wanaume wale walifumba macho na kuziba masikio yao hadi wanaondoka madarakani, waliacha ligi ya miezi sita inachezwa na miezi sita wachezaji wamelala majumbani kwao na mishahara wakilipwa.

Ligi imekuwa ikianza Agosti na Novemba inasimama hadi mwezi Machi au Februari mwishoni na ikifika Aprili ligi imekwisha.

Ukiangalia hapo mchezaji anakuwa uwanjani kwa muda wa miezi isiyozidi sita, halafu tunajidanganya kuwa tunaiga mfumo wa Uingereza ambao wenyewe wakianza ligi Agosti hawasimami hadi Mei 15.

Mpaka inafikia kusimama, wachezaji wanakuwa wamecheza michezo 38 ya ligi, achilia makombe mengine.

Ndiyo maana nilipigia mno kelele jambo hilo na adhabu yake niliipata lakini bora iwe hivyo kwa maslai ya taifa.

Uongozi mpya ulioingia madarakani chini ya Jamal Malinzi uliunda kamati zake nyingi, mojawapo ya kamati iliyonivutia ni ile ya kutengeneza mfumo wa ligi inayoongozwa na Profesa Mshindo Msolla.

Nilipiga hodi ofisini kwa Msolla na kumwonyesha kukerwa kwangu na mfumo uliopita na nilikuwa na kitabu changu cha zamani kidogo, nilimwonyesha mfumo wa ligi na ratiba za ligi kuanzia ligi daraja la pili hadi ligi ya Muungano za mwaka 1986-1990, jinsi wachezaji wetu walivyokuwa wakicheza mechi nyingi na kwa muda mrefu jambo ambalo wachezaji wa leo wamelikosa.

Ndiyo maana nasema naisubiri kwa hamu ratiba hiyo kama itakuwa kama ile iliyopita, basi soka litazidi kwenda kuzimu.

Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) linasema ili mchezaji afikie kiwango cha kimataifa yaani cha ushindani ni lazima acheze mechi zisizopungua 40 kwa msimu mmoja, sasa ni lazima tujiulize wachezaji wetu wanacheza mechi ngapi kwa msimu kama siyo 26 tu.

Kama mchezaji atachaguliwa Taifa Stars atakuwa hajafikia idadi ya michezo kwa upungufu wa michezo 14, lazima awe kichekesho tu.

Nilimwonesha Msolla ligi ilipokuwa ikichezwa kwa miezi tisa bila ya kusimama na hata kama Taifa Stars ilikuwa na michuano ligi yetu ilikuwa ikiendelea kasoro ile timu yenye wachezaji zaidi ya watatu.

Ratiba inaonesha ikiisha ligi yetu inakuja Ligi ya Muungano, halafu Kombe la Taifa ‘Taifa Cup’ yaani michuano ya mikoa ambayo haikuwazuia wachezaji wa ligi kuu kucheza.

Hatimaye bingwa wa ligi kuu anakwenda katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na Afrika Mashariki na ya Kati (Cecafa) akiwa vizuri na wachezaj wameiva kwelikweli.

Nilimthibitishia Msolla itakapofika suala la kujadili mfumo kama unadhani mawazo yangu ni sahihi aniite kwenye kamati kimyakimya na sihitaji posho yeyote, nije nitoe mawazo yangu.

Tunahitaji ligi bora na si bora ligi. Inasikitisha kuwaona akian Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Joseph Owino, Donald Mosoti, Hamis Kiiza na wengineo wa nje wanakaa muda mrefu katika nchi zao tofauti na sisi.

Timu zinaingia mikataba mikubwa na minono kwa wachezaji wao lakini matumizi yao ni kipindi kifupi mno, haingii akilini uwe na kampuni na umwajiri mfanyakazi wako afanye kazi miezi sita na sita kalala kwa mkewe au mumewe halafu umlipe mshahara wa mwaka mzima utegemee kupata faida haiwezekani.

Ndiyo maana leo nasema mazuri mengi mno aliyoyafanya Tenga ambayo Malinzi inabidi ayaendeleze lakini kwangu mimi hili kama TFF italiendeleza hili miye nitatoa shilingi yangu.