Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morrison Simba kuchomokea hapa

KANUNI za Ligi Kuu Bara msimu huu zinamuweka katika uwezekano mkubwa winga wa Simba, Bernard Morrison kukwepa adhabu kutokana na kosa la utovu wa nidhamu licha ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka klabu yake ndio ianze kuchukua hatua.

Mghana huyo, hivi karibuni ameonekana katika kipande cha video akionyesha ishara ya kidole cha kati, akidai anakielekeza kwa watu wanaomchukia jambo ambalo limetafsiriwa kuwa ni tusi.

Kumekuwa na hisia tofauti juu ya kosa hilo ambapo baadhi wanaamini anapaswa kuadhibiwa na wengine wakiamini hatakiwi kuwajibishwa kwa vile limefanyika nje ya uwanja lakini kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu zinamuweka matatani nyota huyo wa zamani wa Yanga.

Ibara ya tano ya kanuni ya 39 ya udhibiti kwa wachezaji, imeorodhesha makosa ambayo yatapelekea mchezaji afungiwe na kutozwa faini, mojawapo likiwa ni kutukana. Hata hivyo kanuni hiyo haijaonyesha kuwa adhabu hiyo inaweza kumhusu mchezaji aliyefanya kosa akiwa nje ya mazingira ya mchezo.

“Mchezaji atakayefanya jambo lolote kati ya yafuatayo atafungiwa michezo isiyopungua mitatu (3) na faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000/-). (5.1) Kutojiunga na timu ya taifa kwa sababu yoyote isiyo ya msingi. (5.2) Kupigana/kupiga kabla, wakati wa mchezo au mara tu baada ya mchezo kumalizika. (5.3) Kumshambulia mwamuzi, kiongozi, mtazamaji au mtu yoyote kwa namna yoyote ile, iwe kwa matusi au kwa vitendo.

(5.4) Kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani,

kukataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa au kuonesha ishara inayoashiria matusi. (5.5) Kufanya vitendo vyenye kuonesha imani za ushirikina na uchawi hadharani au vitavyobainishwa kwa ushahidi mwingineo.(5.6) Kufanya kitendo chochote kingine kitakachobainika kuwa ni kinyume cha maadili ya mchezo wa mpira wa miguu,” inafafanua kanuni hiyo.


WASIKIE WADAU

Mchambuzi wa soka wa kituo cha redio cha EFM, Geoffrey Lea alisema kosa lililofanywa na Morrison lina athari kubwa kwa soka la Tanzania na mchezaji huyo anatakiwa afungiwe na TFF na klabu yake. “Morrison anatakiwa kuadhibiwa na Simba ndio walitakiwa kuwa wa kwanza kumuadhibu. Morrison ni mchezaji wa wastani na Simba ni kama walijipa hasara za bure kumsajili,” alisema Lea.

Naye kocha wa zamani wa Pamba, Muhibu Kanu alisema kitendo cha Morrison hakipaswi kufumbiwa macho na mchezaji huyo anatakiwa kuadhibiwa. “Hakuna kocha anayeunga mkono nidhamu mbovu. Sijajua alikua na maana gani. Morrison ni ‘role model’ (mfano bora), mchezaji ghali wa kigeni.