#LIVE: Ibada mazishi ya Magufuli
Muktasari:
- Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ataongoza viongozi wa Serikali, majeshi ya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, dini na wananchi wa mkoa wa Geita katika mazishi ya hayati John Magufuli, atakayezikwa katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato.
Chato. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ataongoza viongozi wa Serikali, majeshi ya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, dini na wananchi wa mkoa wa Geita katika mazishi ya hayati John Magufuli, atakayezikwa katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato.
Kifo cha Magufuli kilitokea saa 12.00 jioni, Machi 17, mwaka huu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo.