Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC tatizo lipo hapa tu!

Azam FC tatizo lipo hapa tu!

MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba tayari atakuwa ameanza maisha mapya ya nje ya ajira akiwa kwao Romania hii inatokana na wiki moja iliyopita kutimulia katika ajira yake ndani ya klabu hiyo.

Tayari jina la kocha wa zamani wa Zesco United ya Zambia na Yanga, George Lwandamina limekuwa likitajwa kuja kumrithi Mromania huyo aliyeiongoza Azam katika mechi 50 na kushinda 28, sare 11 na kupoteza kwa idadi kama hiyo kabla ya kufurushwa.

Kutimuliwa kwa Cioaba lilikuwa ni jambo linalotabirika, kuwa kama angepoteza pointi tatu mbele ya Yanga basi hatua iliyofuata ni kocha huyo kupoteza ajira hesabu za macho zilionyesha hivyo. Vipigo viwili kutoka kwa Mtibwa Sugar na kisha kugongwa na KMC kulishatoa ishara mbaya kwa Ciaoba na mechi ya Yanga ilikuwa kama fainali yake na kwa bahati mbaya alifeli.

Kuondoka kwa Cioaba wengi wanadhani huenda ndio itakuwa suluhisho ya kuirudisha Azam katika njia kuu ya kuchukua mataji, lakini kwa kuangalia kwa jicho la ziada ni kwamba klabu hiyo inahitaji tiba kubwa zaidi ya kumuondoa Mromania huyu.

Ingawa haisemwi, lakini ukweli ni kwamba kuna matatizo mengi ndani ya Azam na hata kama leo atakuja Jose Mourinho au hata Pep Guardiola bado watapitia magumu na kujikuta wanapoteza kazi ndani ya klabu hiyo ingawa inaonyesha ni klabu yenye kila kitu.

Kiuhalisia ni kwamba Azam inahitaji mafanikio yanayolinga na uwezekaji iliyofanya, lakini bila kutatua yaliyopo ni wazi, mambo yatakuwa ni yale yale na hapa nchini ni vitu ambavyo vinapaswa kuwekwa sawa ili gari la Azam FC likimbie kwa kasi itakayowafikisha mapema kwenye safari yao.

MABOSI WA JUU

Inaelezwa, shida kubwa ya kwanza ya Azam ni viongozi wake wa juu, vigogo wa Azam ambao wengi wao wako katika ngazi ya Ukurugenzi wameshindwa kuishi na mipaka ya nafasi zao baadhi yao wamekuwa makocha na hata watendaji na kwamba anaweza kuja kutamka mtu kitu asiposikilizwa safari ya mtu kuondolewa inaanzia hapo.

Inajulikana Azam ni klabu ya watu binafsi lakini kama hakutakuwa na kuheshimu mipaka ya kazi kwa vigogo hao wa juu na wale wa chini yake taasisi ya namna hiyo lazima itakuwa na kuyumba kwingi kuliko kufanikiwa. Vigogo wa juu wanatakiwa kuacha kufanya kazi kwa kuangalia mtazamo wao au maneno wanayoletewa yana kina gani cha usahihi vinginevyo safari ya kuondoa makocha kila kukicha itaendelea.

USWAHIBA NI TATIZO

Shida nyingine iko hapa Azam kuna baadhi ya vigogo wakubwa wamejenga kasumba ya kuwa na urafiki uliopitiliza na baadhi ya wachezaji, urafiki huo wakati mwingine umekuwa na maneno mengi ya uchochezi ni rahisi kusikia mchezaji amekwenda kumchongea flani kwa uongozi wake na hilo likabebwa kwa uzito.

Aina hiyo ya maisha haiwezi kuwa na afya kwa klabu kubwa kama hiyo, kwani inatengeneza matabaka na pia wakatui mwingine ndio kinachowaondoa baadhi ya makocha na hata wachezaji hata kama hakuna sababu ya kuwaondoka kikosini.

Hata harufu ya kuondolewa kwa Cioaba ilishasikika kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wachezaji wakidai kocha hamalizi wiki swali utakalojiuliza wachezaji kama hao wanaingiaje katika vikao vya viongozi wa juu? Maana halisi hapo ni kwamba inathibitisha kwamba wapo viongozi tayari walishasambaza taarifa hizo kwa wachezaji na hili linatokana na uswahiba ambao unaondoa weledi.

MAKUNDI KWA WACHEZAJI

Lipo kundi au kikundi cha wachezaji wenye nguvu kuliko wengine ndani ya Azam na wengi ni wale wachezaji waliokaa kwa muda mrefu ndani ya klabu nao wamekuwa wakubwa kuliko makocha na hata watendaji wa juu yao.

Kundi hili la wachezaji nilishawahi kutahadharisha huko nyuma kwamba linaweza kuleta shida baadaye, sasa wamekuwa ni zaidi ya makocha na wakati mwingine hata kuthubutu kutaka kuona flani anacheza au flani asicheze na kocha akikataa tu basi aanze kusafisha mabegi yake wakati wowote kazi hana.

Azam kama inataka kupata mafanikio lazima wajue kuwapa nafasi ya usawa wachezaji wote na hata kama kutakuwa na tofauti haitakiwi kuwa kubwa kuliko hali ambayo ipo sasa itapunguza kasi ya mafanikio kwa klabu hiyo.

NINI KIFANYIKE?

Mchakato wa kumpata kocha mpya Azam umeanza, huku jina la Lwandimina likitajwa, lakini ni vyema kwanza Azam ikafanya usafi wa maana wa kuondoa uchafu wote kabla ya kumpokea kocha mpya.

Hatua ya kwanza ya kufanyika, lazima viongozi wa juu katika ngazi ya Bodi ya Wakurugenzi wajue nafasi yao pamoja na kuheshimu nafasi za wale wa chini yao.

Wakubwa hawa wajue kabla ya wao kuanza kufuatilia yale yanayoendelea chini wanaotakiwa kuhojia ni wasaidizi wao Mwenyekiti Shani Christom, Makamu wake Omari Kuwe na Mtendaji Mkuu Abdulkarim Amin ‘Popat’ ambao nao kabla ya matatizo hayajakwenda juu lazima wajue kipi kinaendelea chini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua.

Ndani ya Azam lazima kama kuna mlezi wa timu basi atambue nafasi yake na kufanya majukumu yake kuliko naye kuwa nafasi ya kuamua flani aondoke au huyu hafai wakati jambo husika halijafuata mtiririko mzuri wa kutafutiwa suluhisho. Hili haliwezi kuwa gumu kutekelezeka ndani ya Azam kwa kuwa wapo watu makini katika unyoofu wa uongozi hasa wa soka kama Nassoro Idrissa ambaye uwepo wake ndani ya Bodi ya Wakurugenzi unaweza kuwa msaada wa wakubwa wake wa juu kuweza kujipa nafasi katika maamuzi ya ndani ya klabu yao. Azam bado ina nafasi ya kurudi katika mstari na kurudisha ushindani ulio bora na hata kuchukua mataji