Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia wanavyoteketeza mkwanja juu ya kichwa cha Silva

ATM Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa matajiri wa Saudia wameweka mezani ofa nono sana kuhakikisha inamshawishi fundi huyu akubali kujiunga nao mwisho wa msimu mkataba wake utakapokuwa unamalizika.

MANCHESTER, ENGLAND: MWISHONI mwa wiki iliyopita, jina la Bernardo Silva lilitajwa sana akihusishwa na mpango wa kutaka kuondoka Manchester City, huku ripoti zikidai anaweza kwenda Italia, Hispania au Saudi Arabia.

Inaelezwa matajiri wa Saudia wameweka mezani ofa nono sana kuhakikisha inamshawishi fundi huyu akubali kujiunga nao mwisho wa msimu mkataba wake utakapokuwa unamalizika.

Ikiwa dili hilo litafanikiwa Silva ataingia katika orodha ya wachezaji anaolipwa zaidi duniani kwa sasa na pengine kuongeza utajiri wake. Hapa tumekusogezea ATM yake kufahamu pesa na utajiri alionao kwa sasa na namna atakavyokuwa bwanyenye zaidi ikiwa atatua Saudia.

AT 05

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa, Bernardo Silva anapata mshahara unaofikia Pauni 300,000  kwa wiki ambao ikiwa pamoja na bonasi hufikia Pauni 320,000 kwa wiki.

Mbali na mshahara wa klabu, Silva pia anapata pesa kutokana na mikataba mbalimbali ya udhamini wa kampuni alizosaini.

Kwa sasa ni balozi wa kampuni ya Nike na EA Sports ambazo kwa mwaka zinamwingizia takribani Pauni 4 milioni.

Mbali ya Nike na EA, staa huyu pia inadaiwa ana maduka ya vifaa vya michezo huko Ureno ikiwa ni biashara yake binafsi.

Vilevile ni balozi wa kampuni ya masuala ya kifedha ya Axi Partnership ambayo inamlipa takribani Pauni 5 milioni kwa mwaka.

AT 02

MIJENGO

Bernardo anaishi katika nyumba ya kifahari jijini Manchester yenye thamani ya Pauni 5 milioni ambao ndani una Gym binafsi, kiwanja kidogo cha kufanyia mazoei ya mpira wa miguu.

Pia kuna sehemu ya mapumziko, Bwawa dogo la kuogelea na Bustani yenye mandhari ya kisasa.

Vilevile anamiliki nyumba nyingine nchini kwao Ureno inayokadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 2 milioni.

AT 01

NDINGA

Audi RS7 – Pauni 100,000

Mercedes-Benz G-Class – Pauni 120,000

Porsche Panamera – Pauni 90,000

Ferrari F8 Tributo – Pauni 250,000

BMW M8 – Pauni 120,000

Mbali na magari, Bernardo pia anapenda kuendesha pikipiki na anamiliki mbili kwa sasa.

AT 04

MSAADA KWA JAMII

kutokana na taasisi mbalimbali za kijamii, Silva amekuwa akichangia msaada wa elimu kwa vijana wasio na uwezo wa kujiendeleza kimasomo.

Inaelezwa kwa maka 2023 pekee, alitumia takribani Pauni 200,000 kwa ajili ya kusaidia miradi ya vijana kwenye elimu na michezo.

AT 03

FAMILIA NA MAISHA BINAFSI

Bernardo Silva yupo katika ndoa na mrembo Ines Tomaz na hadi sasa wana mtoto mmoja wa kike aitwaye Carlota.

Mkewe Tomaz anafanya kazi kama modo na mwigizaji akiwa mmoja kati ya wasanii maarufu Ureno.

Kawaida Silva sio mtu wa kula bata na muda mwingi amekuwa akiutumia zaidi akiwa na familia yake ikiwa hayupo katika majukumu ya timu.