Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cardi B; Tajiri anayefukuzwa Marekani

ATM Pict

Muktasari:

  • Cardi B, ambaye jina lake halisi ni Belcalis Marlenis Almanzar, ni miongoni mwa watu maarufu ambao wanapigiwa kura ili kurudishwa kwenye nchi zao za asili.

NEW YORK, MAREKANI: KUANZIA mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, jina la Cardi B limeendelea kutawala vichwa vya habari duniani, si tu kwa muziki wake bali kwa kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii.

Cardi B, ambaye jina lake halisi ni Belcalis Marlenis Almanzar, ni miongoni mwa watu maarufu ambao wanapigiwa kura ili kurudishwa kwenye nchi zao za asili.

Hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita takribani watu elfu 80, walikuwa wamepiga kura kuunga mkono kuondolewa Marekani kwa msanii huyu kupitia kampeni iliyoanzishwa katika mitandao hiyo.

Mbali ya sakata hilo, leo tumekusogezea undani wa utajiri wake na jinsi anavyopiga pesa.

AT 03

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa, utajiri wa Cardi B unakadiriwa kufikia Dola 80 hadi 90 milioni. Kiasi hiki kinatokana na mauzo ya nyimbo zake, matamasha, udhamini, mitandao ya kijamii pamoja na uwekezaji wake binafsi.

Cardi B amepata umaarufu mkubwa kupitia nyimbo kama Bodak Yellow, I Like It, WAP na Up, ambazo zimemuingizia zaidi ya Dola 70 milioni kupitia mauzo kwenye sekta za  kidijitali.

Albamu yake ya  Invasion of Privacy ilivunja rekodi kadhaa na kumpatia tuzo ya Grammy. Card B ameuza jumla ya nakala milioni saba za albamu hiyo na hadi sasa ndio msanii wa kike aliyeuza albamu nyingi zaidi kwa karne hii.

Mbali na muziki, Cardi B ni miongoni mwa wasanii wanaolipwa fedha nyingi kwenye matangazo ana mikataba ya udhamini na kampuni kubwa kama,  Pepsi, Reebok, Fashion Nova, Balenciaga na Skims

Kupitia mikataba hiyo, anasemekana kuingiza zaidi ya Dola 15 milioni  kwa mwaka.

Vilevile, Cardi B hupata pesa nyingi kupitia akaunti zake za Instagram na TikTok, ambako chapisho moja la matangazo linaweza kumuingizia zaidi ya Dola 1 milioni.

AT 01

MIJENGO

Mrembo huyu anamiliki jumba la kifahari jijini New York, Marekani, lenye thamani ya takribani Dola  5 hadi 6 milioni.

Nyumba hiyo ina vyumba zaidi ya vinane, mabafu ya kisasa, studio ya muziki, bwawa la kuogelea na eneo kubwa la mapumziko.

Vilevile, anamiliki nyumba nyingine ya kifahari huko Los Angeles, ambayo huitumia zaidi kwa mapumziko na kurekodi nyimbo zake. Nyumba hiyo ina thamani ya zaidi ya Dola 4 milioni.

AT 02

MSAADA KWA JAMII

Aliwahi kuchangia zaidi ya Dola 200,000 kusaidia waathirika wa janga la COVID-19 nchini Marekani, pia amekuwa akisaidia familia maskini jijini New York, hasa katika eneo alilokulia la Bronx.

Ameshafanya kampeni za kutoa chakula na misaada kwa waathirika wa majanga ya asili.

AT 04

FAMILIA NA BATA

Cardi B alikuwa kwenye ndoa na rapa Offset (mwanachama wa kundi la Migos) na wakaachana Julai 2024.

Wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Kulture Kiari Cephus, aliyezaliwa mwaka 2018, Wave Set Cephusmwengine alizaliwa mwaka 2021 na Blossom wa mwaka 2024.

Kwa sasa ana mtoto mwingine mdogo wakiume aliyemzaa Novemba na mchumba wake mpya  Stefon Diggs.