Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wake na wapenzi wa makocha wanaovutia

WAPENZI Pict

Muktasari:

  • Kutoka kwa mwanamitindo maarufu wa Uingereza hadi mwigizaji aliyewahi kuonekana katika tamthilia ya CSI: Miami, haya ndiyo maisha ya kimapenzi ya wake na wapenzi wa baadhi ya makocha wakubwa wa soka.

LONDON, ENGLAND: SI wachezaji wa soka pekee wanaopata wapenzi warembo na maarufu. Hata makocha wao wamefanikiwa kupata wenza wanaovutia nje ya uwanja.


Kutoka kwa mwanamitindo maarufu wa Uingereza hadi mwigizaji aliyewahi kuonekana katika tamthilia ya CSI: Miami, haya ndiyo maisha ya kimapenzi ya wake na wapenzi wa baadhi ya makocha wakubwa wa soka.

Tunaanza na mrembo mwenye asili ya Argentina na Hispania.


WAPE 01

LORENA BERNAL

Lorena Bernal, 45, ni mke wa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.

Alianza kazi ya uanamitindo akiwa na umri wa miaka saba, kabla ya kutwaa taji la Miss Hispania akiwa na miaka 17.

Mwaka 2002, alikutana kwa mara ya kwanza na Arteta katika klabu ya usiku mjini San Sebastian, eneo la pwani nchini Hispania.

Lorena pia, amewahi kujihusisha na uigizaji, akionekana katika vipindi vya televisheni vya Marekani kama Chuck na CSI: Miami.

Yeye na Arteta wana watoto watatu wa kiume ambao ni Gabriel, Daniel na Oliver.


WAPE 02

LUCY PINDER

Lucy Pinder, aliyewahi kuwa mwanamitindo maarufu katika majarida ya FHM na Nuts, alianza uhusiano na kocha wa sasa wa Leicester City, Russell Martin, karibu Juni 2024.

Waliweka wazi uhusiano wao miezi kadhaa baadaye, wakati Lucy alipoandamana na Martin katika Chuo Kikuu cha Brighton, ambako kocha huyo alitunukiwa shahada ya heshima.

Mwezi Februari mwaka huu, baada ya kuwa pamoja kwa takribani miezi 18, wawili hao walitangaza kuwa wamefunga ndoa.

Mbali na kazi yake ya upigaji picha za kimtindo, Lucy, ambaye sasa ana miaka 42, pia amewahi kushiriki katika kipindi cha Celebrity Big Brother pamoja na filamu kadhaa zilizotengenezwa na kampuni huru.


WAPE 03

KARO BERGER

Mwigizaji na mwanamitindo Mjerumani Anna Karolin Berger, anayefahamika kwa kifupi kama Karo kwenye mitandao ya kijamii, hivi karibuni aliweka wazi uhusiano wake na kocha wa Brighton, Fabian Hurzeler.

Anna, anayeishi Munich, kwa sasa anaigiza katika tamthilia maarufu ya Ujerumani Sturm der Liebe (Love Storm).

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 ameshiriki katika filamu na vipindi mbalimbali vya televisheni tangu alipoanza kuonekana kwenye skrini mwaka 2017, baada ya awali kufanya kazi katika sanaa ya maigizo ya jukwaani.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa Anna na Hurzeler wamekuwa katika uhusiano wa mbali kutokana na majukumu yao.


WAPE 04

DANIELLA SEMANN FABREGAS

Daniella Semaan Fabregas, sasa mwenye miaka 51, aliwahi kuitwa “Malkia wa Wags” wakati mumewe, Cesc Fabregas, alipokuwa akiichezea Chelsea.

Mrembo huyo mwenye asili ya Lebanon na mama wa watoto watano alikutana na nyota huyo wa zamani wa Hispania mwaka 2011 katika mgahawa wa Kijapani uliopo Knightsbridge, London.

Daniella amewahi kueleza kuwa alimsogelea Cesc alipokuwa amekaa mezani na kumuomba autograph kwa ajili ya mwanawe Joseph, ambaye ni shabiki mkubwa wa soka. Baada ya hapo, wawili hao walibadilishana namba za simu.

Kwa sasa wanaishi maisha yao mjini Como, Italia, ambako Cesc mmoja wa mastaa wa zamani wa Ligi Kuu England, anafundisha soka.

Daniella pia ni rafiki wa karibu wa Antonela Roccuzzo, mke wa Lionel Messi.


WAPE 05

CHRISTINE LAMPARD

Christine alikutana na kocha wa Coventry City, Frank Lampard, mwaka 2009 katika hafla ya Pride of Britain Awards.

Walifunga ndoa miaka sita baadaye mbele ya ndugu na marafiki katika Kanisa la St Paul’s, Knightsbridge. Sherehe za ndoa zilifanyika katika klabu binafsi ya wanachama, The Arts Club.

Christine, mwenye miaka 47, na Frank wana watoto wawili, binti aliyezaliwa mwaka 2018 na mtoto wa kiume aliyezaliwa mwaka 2021.

Christine anafahamika zaidi kama mtangazaji wa televisheni, akiwahi kuonekana katika vipindi kama The One Show na Loose Women.


WAPE 06

RACHEL MASON

Rachel Mason, 34, alikutana na Ryan Mason ambaye hivi karibuni alikuwa kocha mkuu wa West Brom wakati akisoma biashara na uchumi katika Chuo Kikuu cha Lancaster.

Rachel alisimama na Ryan wakati alipoumia vibaya kichwani mwaka 2017, jeraha lililokuwa hatarishi kwa maisha yake na hatimaye kumlazimisha kustaafu soka la ushindani.

Wawili hao wana watoto watatu mmoja mwanaume aliyezaliwa mwaka 2017 na mabinti wawili waliozaliwa mwaka 2019 na 2023.

Walifunga ndoa katika kisiwa cha Mallorca, Hispania, Juni 2022.


WAPE 07

NAGORE ARANBURU

Nagore Aranburu, 46, na mumewe, kocha wa Chelsea Xabi Alonso, ni wapenzi tangu utotoni.

Kama ilivyokuwa kwa Arteta na Lorena, wawili hao walikutana wakiwa vijana mjini San Sebastian, kabla ya kufunga ndoa mwaka 2009.

Miezi kadhaa baadaye, Alonso, ambaye wakati huo alikuwa kiungo wa zamani wa Liverpool, aliondoka Anfield pamoja na mkewe kuelekea Real Madrid.

Nagore alianza kama mwanamitindo kabla ya kuingia katika ubunifu wa mavazi, na amekuwa akimuunga mkono Alonso katika safari yake yote ya soka.

Wawili hao wana watoto watatu ambao ni Jon, Ane na Emma.


WAPE 08

EMMA SAUNDERS

Emma Saunders mtangazaji wa Sky Sports mwenye miaka 33, yuko kwenye uhusiano na kocha wa sasa wa Auxerre, Will Still.

Wawili hao waliuweka wazi uhusiano wao kwenye Instagram mwaka 2024, walipoonekana pamoja wakihudhuria mchezo katika michuano ya Euro 2024.

Hata hivyo, mwanzoni mwa mwaka 2025, Emma alikumbwa na changamoto kubwa kiafya baada ya kugundulika kuwa na saratani ya tezi pamoja na maambukizi ya virusi yaliyosababisha ugonjwa wa encephalitis, hali iliyomfanya apoteze fahamu na kuingia katika koma.

Will aliamua haraka kuacha kazi yake katika klabu ya Ufaransa, Lens, ili kuwa pembeni ya Emma wakati huo mgumu.

Emma baadaye alirejea katika kazi yake ya Sky Sports mwaka 2025, ambapo katika mahojiano yenye hisia alitoa shukrani kwa Will kwa msaada aliompa wakati wa kipindi hicho kigumu.