Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uteuzi wa Kizuguto TFF ni kituko kingine cha mwaka mpya

Muktasari:

Ni kawaida kwa watawala wetu kufikiria kwa akili ya jana kutatua matatizo ya leo. Ni jambo ambalo linasikitikisha kwa sababu wote tumekubali hali hiyo na tumeona ni hali ya kawaida.

DUNIA huwa haiishi vituko na hayo ndiyo mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kila siku na bado tutaendelea kuyaona miaka mingi ijayo.

Ni kawaida katika nchi za dunia ya tatu kama Tanzania, ambako watu waliosababisha matatizo ndiyo haohao hutumika kutatua matatizo.

Ni kawaida kwa watawala wetu kufikiria kwa akili ya jana kutatua matatizo ya leo. Ni jambo ambalo linasikitikisha kwa sababu wote tumekubali hali hiyo na tumeona ni hali ya kawaida.

Kwa hali ilivyovurugika katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unahitaji watu makini kuleta mabadiliko katika idara zote za shirikisho hilo.

Huhitaji watu wa kubabaisha wala watu ambao hawana weledi katika kazi zao. Huhitaji watu ambao wataleta matatizo zaidi katika shirikisho hilo.

Unahitaji watu wa aina ya Boniface Wambura, ambaye utendaji wake wa kazi huwezi kuwa na shaka nao hata kidogo.

Tumesikia uteuzi wa ofisa habari wa zamani wa Yanga, Baraka Kizuguto kuteuliwa kushika wadhifa huo TFF.

Haya ni majanga mengine kwa sababu, mtu ambaye Yanga hawakutaka kuendelea naye kwa sababu wanazozijua wao, inakuwaje anakwenda kuwa ofisa habari wa TFF kuvaa viatu vya Wambura?

Kizuguto, ambaye akiwa Yanga alikosa ushirikiano na waandishi wa habari hata kukwaruzana mara kadhaa, hafai kushika wadhifa huo, labda kama amepewa kwa sababu ya kubebana.

Kwa muda ambao Wambura amekuwa akifanya kazi hiyo TFF, tumeshuhudia weledi wa hali ya juu, utendaji wake wa kiwango cha juu na uhusiano na vyombo vya habari na wadau wengine ulikuwa hauna tatizo.

Hali hiyo haiwezi kutokea tena, kwa sababu Kizuguto ambaye hupenda kuingilia siasa za mpira na fitina, bila shaka hawezi kuacha hilo na ataendelea kufanya kama alivyokuwa akifanya Yanga na sioni kama kutakuwa na uhusiano mzuri na waandishi wa habari.

Ukiacha sifa yake ya kupenda kuficha habari badala ya kuzitoa, Kizuguto akiwa Yanga aliwashawishi makocha kutozungumza na waandishi badala yake akataka hata mambo ya kiufundi yeye ndiye awe anazungumza, akataka hata maswali ya fomesheni uwanjani yeye ndiye aulizwe badala ya kocha.

Licha ya kwamba hana taaluma ya uandishi wa habari, ni mtu ambaye anataka kuonekana zaidi na kwa hilo tu, sidhani kama ataweza kuvaa viatu vya Wambura.

Miaka mitatu iliyopita, mwandishi wa Mwanaspoti Michael Momburi akiwa ameambatana na kikosi cha Yanga kambini Uturuki, alitimuliwa kama mbwa akiwa nchi ya ugenini baada ya Kizuguto na mkuu wa msafara wa Yanga kushirikiana kumfukuza.

Kilikuwa ni kitendo cha aibu, cha kinyama na ambacho itachukua miaka mingi katika maisha yangu kukisahau na hasa ikizingatiwa kuwa hakuna kosa lolote ambalo mwandishi huyo alikuwa amefanya.

Kwa bahati mbaya sana, Kizuguto hakujua kuwa hilo lilikuwa ni jambo la kupita. Hakujua kuwa kuna siku historia itakuja kumhukumu. Sijui anaweza kujitetea vipi kwa unyama huo ambao aliufanya Uturuki kwa Mtanzania mwenzake?

Mwaka jana, wakati Yanga ikiwa katika malumbano na Azam TV, kuna siku Kizuguto aliongoza kikundi cha makomandoo wa Yanga kuwafanyia vurugu wapigapicha wa Azam TV ili wasifanye kazi yao katika Uwanja wa Taifa.

Badala ya kufanya kazi yake ya kuwa ofisa habari alijihusisha katika mambo yasiyomhusu na ndiyo maana haikuwa ajabu kuona akihusika katika kuhesabu fedha zilizotokana na viingilio milangoni. Kama anataka kufanya kazi TFF anatakiwa kubadilika sana, tena sana, aache kudhani anajua kuliko watu wengine, asidhani watu waliokaa kimya hawajui? Afanye kazi yake kwa weledi. Namtakia kila la kheri katika majukumu yake TFF.