Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugumu wa kuwatetea marefa wanaoharibu mechi kizembe

MAREFA Pict

Muktasari:

  • Sasa kwa mfano yalipokuja masuala ya video kwa ajili ya kuwasaidia kuchezesha, hapa kijiweni tuliamini mambo yatakuwa mswano na uamuzi usioeleweka utapungua.

Yaani kuna wakati sijui ndiyo huwa wanaamua kutrendi maana wanafanya vitu ambavyo kikawaida hutegemei kuona wakivifanya lakini wao ndo huamua kwenda navyo mjini.

Sasa kwa mfano yalipokuja masuala ya video kwa ajili ya kuwasaidia kuchezesha, hapa kijiweni tuliamini mambo yatakuwa mswano na uamuzi usioeleweka utapungua.

Kwa maana watapata nafasi ya kuangalia kwa utulivu tukio lenye utata na sintofahamu kisha watalitolea uamuzi na sio kama ilivyokuwa zamani na walikuwa wanasingizia eti ni makosa ya kibinadamu.

Na walianza vizuri kweli msimu huu kwa jinsi walivyotumia video kufanya uamuzi ambao ulisababisha wengi tuwapongeze na kuacha kuwapa lawama na tukaamini sifa hizo zitawafanya wajitahidi kuchezesha vizuri zaidi.

Cha ajabu sasa wameanza kutaka kuturudisha kulekule ambako tulikuwa tunapakataa ambako ni kutoa uamuzi unaoacha shaka kwenye mechi.

Baadhi wameanza kutoa kadi zisizostahili kama ile nyekundu aliyopata Gibrill Sillah katika mechi ya Ligi dhidi ya Kagera Sugar. Eti anamiliki mpira akamgonga kwa mkono mchezaji wa Kagera kwa bahati mbaya lakini refa akampa nyekundu.

Haya kuna wengine wao wameamua kulea kupoteza muda. Mechi unakuta muda umepotea mwingi kutokana na matukio mbalimbali lakini wanaongeza dakika chache tu.

Shauri yao wenyewe bhana inaonekana wanapenda na wameshazoea maisha ya kusimangwa na kulaumiwa kila wakati.