Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF mambo yote yapo Tanga

TANGA Pict

Muktasari:

  • Ndio, kama hujui leo Jumamosi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linafanya Uchaguzi Mkuu kusaka viongozi wapya wa kuliongoza shirikisho hilo, ambapo wagombea 11 wakijiandaa kupigiwa kura.

LICHA ya ukweli usiku wa leo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa uwanjani kukamilisha ratiba ya mechi za Kundi B ya michuano ya CHAN 2024, lakini macho na masikio ya wadau wa soka watayaelekeza jijini Tanga.

Ndio, kama hujui leo Jumamosi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linafanya Uchaguzi Mkuu kusaka viongozi wapya wa kuliongoza shirikisho hilo, ambapo wagombea 11 wakijiandaa kupigiwa kura.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita uliofanyika Agosti 7, 2021 pia jijini Tanga, nafasi ya Urais ina mgombea mmoja, Wallace Karia anayetetea kiti kwa mara nyingine, huku wagombea 10 wanachuana kuwania nafasi sita za ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo.

Uchaguzi huo unafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi ya leo, huku kukiwa na kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu kupinga mchakato wake, baada ya awali kupingwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) bila mafanikio (jana ilikuwa ikiendelea kusikilizwa, jijini Dar es Salaam).

Kabla ya wagombea hao 11 kupenya katika orodha ya mwisho, jumla ya wagombea 25 walijitokeza kuwania nafasi zinazowaniwa wakiwamo wagombea sita wa urais na wengine 19 wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambao hata hivyo kanuni ya udhamini (endorsment) iliwaengua baadhi yao mapema.

TANG 03 (1)

WAPIGA KURA

Katika uchaguzi huo kutokana na marekebisho ya katiba, wapiga kura 83 ndio wenye jukumu la kuamua hatma ya TFF mpya katika Uchaguzi Mkuu huo.

Wajumbe hao watakaoshiriki kupiga kura katika uchaguzi huoni pamoja na Wajumbe 16 wa klabu za Ligi Kuu Bara ambazo zitawakilisha na mjumbe mmoja mmoja.

Pia kuna wajumbe 52 kutoka Vyama vya Mikoa 26 ambavyo vitawakilishwa na wapiga kura wawili kwa kila moka na kufanya idadi iwe ni 52, sambamba na Wajumbe 15 wa vyama vitano shirikishi.

Vyama hivyo shirikishi ni;  Chama wa Waamuzi Tanzania (FRAT), Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), Chama cha Madaktari wa Michezo (TSMA), Chama cha Wachezaji (SPUTANZA) na Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) vinavyotoa wajumbe watatu wa kupiga kura.

TANG 03

NAFASI SABA TU

Katika uchaguzi huo nafasi saba tu nduizo zinazowaniwa na wagombea 11 waliopitishwa ikiwamo moja ya urais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Sita tofauti  za kimkoa kisoka.

Kanda hizo ni ile namba moja yenye mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro na Pwani, kanda namba mbili yenye Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga wakati kanda namba tatu ni mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Songwe.

Kanda namba nne ina mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Singida, huku kanda namba tano ina mikoa ya Geita, Mara, Mwanza na Kagera na kanda namba sita inaunganisha mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa na Tabora.

TANG 01

WAGOMBEA

Ukiacha nafasi ya urais yenye mgombea mmoja tu, Wallace Karia anayetetea kiti baada ya waliojitokeza kupambana nao kuchomolewa mapema kwa kuzingatia mabadiliko ya Kanuni za Uchaguzi wa TFF ya mwaka 2021, katika ujumbe wa utendaji ina wagombea 10.

Wagombea hao wanachuana kupitia kanda sita, huku kanda tatu tofauti zikiwa zina mgombea mmoja mmoja, tofauti na kanda nyingine tatu pia zenye wagombea zaidi ya mmoja.

Katika kanda namba moja yenyewe ina wagombea wawili akiwamo anayetetea kiti Lameck Nyambaya anayechuana na Hosea Lugano, huku Kanda Namba mbili ina mgombea mmoja tu, Khalid Abdallah Mohammed kama ilivyo kwa  Kanda namba nne yenye kuwaniwa na Mohammed Aden na ile ya namba sita yenye mgombea pekee, Issa Bukuku.

Kanda Namba Tatu yenyewe ina wagombea watatu ambao ni James Mhagama, Evance Mgeusa na Cyprian Kuyava wakati kanda namba tano nayo ikiwa na wagombea wawili, Vedastus Lufano na Salum Kulunge.


MATOKEO YALIYOPITA

Katika uchaguzi uliopita uliomrejesha Karia madarakani kwa mara ya pili Agosti, 2021 alipigiwa kura za ndio na wajumbe 81 ikiwa ni sawa na asilimia 100 baada ya awali kushika nafasi hiyo kupitia uchaguzi wa mwaka 2017 na kuwashinda wapinzani aliochuana nao katika kinyang’anyiro hicho.

Uchaguzi wa 2017 Karia alipata jumla ya kura 95 kati ya 127 zilizopigwa na wajumbe akiwashinda wagombea wengine ambao kura zao zipo kwenye mabano; Emmanuel Kimbe (1), Frederick Mwakalebela (3), Imani Madega (8), Richard Shija (9) na Ally Mayai (9).

Huku Nafasi ya Makamu wa Rais iliyokuwapo kipindi hicho kabla ya mabadiliko ya katiba ilitwaliwa na Michael Wambura aliyeshinda nafasi hiyo kwa kupigiwa kura 85, huku wajumbe 12 kutoka Kanda 12 walipenya katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

Hata hivyo, katika uchaguzi uliofuata wa mwaka 2021 kanda hizo zilipunguzwa na kuwa sita zikiunganisha mikoa ambayo safari hii pia wanachuana katika mfumo huo na wapiga kura ndio watakaoamua nani waingie katika safu mpya ya TFF itakayodumu kwa miaka minne ijayo.