Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kifo cha Keegan na nguli Omar Hussein wa Yanga

KEAGAN Pict

Muktasari:

  • Omar Hussein alianza kulinganishwa na Keegan alipojiunga na Yanga mwaka 1976 akitokea Mseto ya Morogoro.

KIFO cha nguli wa soka wa England, Kevin Keegan, kimeibua kumbukumbu za mshambuliaji wa zamani wa Yanga na baadaye Simba, Omar Hussein, ambaye aliwahi kupewa jina la utani la "Kevin Keegan" kutokana na uchezaji wake kufanana na wa nyota huyo wa England.

Omar Hussein alianza kulinganishwa na Keegan alipojiunga na Yanga mwaka 1976 akitokea Mseto ya Morogoro.

Kipaji chake kilimpa nafasi ya kuitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania akiwa na umri wa miaka 19, huku mafanikio yake makubwa kimataifa yakijumuisha kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 1980 nchini Nigeria.

Ingawa Omar Hussein kwa sasa amestaafu soka, historia yake haiwezi kutenganishwa na jina la Kevin Keegan, ambalo lilimjengea utambulisho mkubwa katika maisha yake ya soka kutokana na ufanano wa mtindo wao wa uchezaji.

Kifo cha Keegan kimefufua kumbukumbu za enzi hizo na urithi aliouacha, si tu nchini England bali pia kwa mashabiki wa soka Tanzania waliomfananisha na mmoja wa nyota wao mahiri.

KEEG 01

KIFO CHA KEEGAN

Keegan ambaye ni nahodha, mchezaji, na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool, Kevin Keegan, amefariki dunia juzi Jumatatu akiwa na familia yake.

Keegan mwenye umri  wa miaka 75 amefariki dunia  baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya hatua ya nne kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolewa na familia yake kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa nguli huyo amefariki dunia akiwa amezungukwa na mkewe, Jean, pamoja na binti zake katika nyakati zake za mwisho.

 Keegan anakumbukwa kama mmoja wa wachezaji bora na maarufu zaidi wa kizazi chake, akiwa mchezaji pekee wa Uingereza kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or mara mbili mfululizo.


KEEG 02

REKODI, USHIRIKI KOMBE LA DUNIA

Kevin Keegan alicheza mashindano ya Kombe la Dunia mara moja tu, ambapo alishiriki kwa dakika 26 pekee katika michuano ya mwaka 1982 nchini Hispania.

Licha ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kizazi chake nchini England na mshindi mara mbili wa tuzo ya Ballon d'Or, maisha yake ya soka kwenye Kombe la Dunia yaligubikwa na bahati mbaya kutokana na sababu kadhaa.

Miongoni mwa sababu hizo England ilishindwa kufuzu katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1974 na 1978, kipindi ambacho Keegan alikuwa kwenye kiwango chake bora zaidi.

Poa, alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya England kuelekea michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1982, lakini kutokana na matatizo ya mgongo lilimfanya akae benchi katika mechi zote za hatua ya makundi.

KEEG 03

MECHI YA PEKEE

Hata hivyo, Keegan alifanikiwa kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba Julai 5, 1982, kwenye mechi dhidi ya wenyeji Hispania na alicheza kwa dakika 26 tu, mechi ikamalizika kwa suluhu ya 0-0, na England ikayaaga mashindano. Hispania ndio mabingwa wapya Kombe la Dunia 2026.

KEEG 04

USHIRIKI NA MAFANIKIO KATIKA LIGI YA ULAYA

Keegan alikuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya klabu ya Liverpool FC katika miaka ya 1970 kabla ya kuhamia klabu ya Hamburger SV ya Ujerumani, ambapo aling'ara sana kwenye mashindano makubwa ya Ulaya.

 Aliiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa wa kihistoria wa michuano hii mwaka 1977 baada ya kuifunga Borussia Mönchengladbach mabao 3-1 kwenye fainali mjini Roma.

 Pia, akiwa na Hamburger SV ya Ujerumani, alicheza fainali nyingine ya Kombe la Ulaya mwaka 1980, ingawa walipoteza kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Nottingham Forest.

KEA 01

KOMBE LA UEFA (SASA UEFA EUROPA LEAGUE)

Keegan alishinda makombe mawili ya UEFA akiwa na Liverpool (mwaka 1973 na 1976) huku akifunga mabao muhimu kwenye mechi za fainali za michuano hiyo.

Idadi ya mabao

Keegan alikuwa mshambuliaji hatari mwenye uwezo mkubwa wa kukimbia na chenga, akifunga jumla ya mabao 206 katika ngazi ya vilabu katika maisha yake yote ya soka.


TIMU YA TAIFA YA ENGLAND

Alicheza mechi 63 na kufunga mabao 21, huku akiwa nahodha wa timu hiyo katika mechi 31.

Akiwa Liverpool FC (1971–1977), alifunga jumla ya mabao 100 katika michezo 323.

HAkiwa Hamburger SV (1977–1980),  alifunga mabao 40 katika michezo 112 nchini Ujerumani.

Southampton na Newcastle United, alifunga mabao 42 akiwa na Southampton ambapo alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 1981-82 kwa mabao 26), na mabao 49 katika michezo 85 akiwa na Newcastle kabla ya kustaafu mwaka 1984.

Baada ya maisha yake kama mchezaji, Keegan alipata mafanikio makubwa pia kama kocha, akiinoa timu ya Taifa ya Uingereza, Newcastle United aliyoiwezesha kupanda daraja na kuwa washindi wa pili wa Premier League 1996), Fulham, na Manchester City.

KEA 02

KUSTAAFU SOKA

Kevin Keegan alistaafu rasmi soka la kulipwa kama mchezaji katika majira ya joto ya mwaka 1984, kufuatia mafanikio makubwa aliyopata akiwa na klabu ya Newcastle United.

Baada ya kutundika daluga, alihamia kwenye kazi ya ukocha ambapo alipata mafanikio makubwa na kuwa mmoja wa mameneja mashuhuri, kabla ya kuhitimisha rasmi safari yake ya ukocha mnamo Septemba 2008 alipoondoka katika klabu yake ya mwisho ya Newcastle United.