Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Roc Nation ya Jay-Z yatikisa soko la usajili Ulaya

ROC Pict

Muktasari:

  • Na karibuni mwishowe mshindi alikuwa wazi. Ushindi wa hivi karibuni wa Jay-Z ulikuja saa 24 tu baada ya mke wake, Beyonce, kutoa wimbo mpya wa Morning Dew (Donk), ambao ilikuwa ni rekodi ya kwanza baada ya miaka minne kwa Jay-Z akirapu.

LONDON, ENGLAND: ROC Nation Sports ya Jay-Z inaanza taratibu kutikisa soko la usajili wa wachezaji Ulaya ikiwa tayari na mastaa wa soka, Vinicius Junior na Yan Diomande kati ya wachezaji zaidi ya 100 wanaowakilishwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na gwiji huyo wa muziki wa hip-hop.

Na karibuni mwishowe mshindi alikuwa wazi. Ushindi wa hivi karibuni wa Jay-Z ulikuja saa 24 tu baada ya mke wake, Beyonce, kutoa wimbo mpya wa Morning Dew (Donk), ambao ilikuwa ni rekodi ya kwanza baada ya miaka minne kwa Jay-Z akirapu.

Siku hizi, mwanamuziki huyo ambaye bado ni miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa hip-hop anajihusisha na biashara mbalimbali kuanzia huduma ya muziki ya Tidal na chapa yake ya mavazi ya mitaani, hadi biashara za shampeni.

RO 01

Hata hivyo, ni Roc Nation Sports, kampuni tanzu ya burudani iliyoanzishwa 2008 ambayo imekuwa ikivutia zaidi katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi.

Roc Nation Sports ilianzishwa miaka mitano baadaye kwa ushirikiano na Creative Artists Agency, na mwanzoni ilijikita zaidi katika kuwasimamia mastaa wa NBA, NFL na MLB, akiwemo Kevin Durant.

Jerome Boateng wa Bayern Munich alikuwa mchezaji wa kwanza wa soka kujiunga nayo  2015, kabla ya kuanzishwa kwa Roc Nation Sports International (RNSI) miaka minne baadaye, ikiwa na lengo la kuwawakilisha mastaa wanaocheza katika klabu kubwa za Ulaya.

RO 02

Ikiwa na makao yake London, kampuni hiyo sasa ina zaidi ya wachezaji 100 kwenye orodha yake akiwemo Vinicius, mshambuliaji wa Brazil ambaye hivi karibuni alisaini mkataba mpya wenye thamani kubwa na Real Madrid unaoaminika kuwa wa takribani Euro 25 milioni kwa mwaka.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Arsenal kuhusishwa na mpango wa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Julai 2023, RNSI ilinunua kampuni iliyokuwa na mafanikio ya mawakala wa Brazil, TFM, ambayo tayari ilikuwa inamwakilisha Vinicius pamoja na Gabriel Martinelli na Endrick, na kuibadili jina kuwa Roc Nation Sports Brazil.

Katika mazungumzo yaliyodumu kwa miaka miwili, kampuni hiyo ilitarajia kuishawishi Real Madrid kuongeza mshahara wa nyota huyo hadi Euro 30 milioni kwa mwaka ili kufikia kiwango cha Kylian Mbappe. Pia iliruhusu mkataba wake kuingia katika miezi 12 ya mwisho, hatua iliyolenga kuchochea klabu zingine kumtaka mchezaji huyo.

RO 03

Arsenal ambayo sasa inapambana kusaka mbadala baada ya Vinicius akiwemo Iliman Ndiaye wa Everton inaaminika kuwa ilikuwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha kumsajili staa huyo.

Hata hivyo, inaeleweka kwamba Arsenal iliuona uwezekano wa kumpata mchezaji huyo bure msimu ujao kuwa mkubwa zaidi. Pamoja na hayo, Real Madrid iliongeza ofa yake na Vinícius akaamua kubaki.

Uamuzi huo unaonekana huenda ukawagharimu nafasi ya kumsajili Rodri kutoka Manchester City, baada ya Barcelona kuanza kujiimarisha katika mbio za kumnasa kiungo huyo kabla ya wapinzani wao wakubwa.

Siku ambapo mkataba mpya wa miaka sita wa Vinícius ulitangazwa, Yan Diomande alisafiri kwa ndege hadi Hispania kukamilisha uhamisho wake wa rekodi wa Pauni 115 milioni kutoka RB Leipzig.

RO 04

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye amecheza mechi 46 pekee katika ngazi ya juu kwa Leipzig na Leganes ya daraja la pili nchini Hispania, tayari amekuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Afrika katika historia. RNSI inaripotiwa kulipwa hadi Pauni 17 milioni kama kamisheni na ada mbalimbali kutokana na dili hilo. Na saga hilo lililodumu kwa muda mrefu lilianza Liverpool ilipokataliwa ofa yake ya Pauni 70 milioni na Leipzig mwezi Juni. Hatimaye Diomande alisaini mkataba wa miaka saba na Real Madrid.

Uhamisho huo umeonyesha kwa kiasi kikubwa namna mchakato wa kisasa wa usajili wa wachezaji unavyofanya kazi, huku kila wiki ukiwa mabadiliko mapya.

Baada ya kuambiwa kwamba ilihitajika kulipa zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumnunua Diomande, PSG ilijiondoa kwenye mbio hizo mwishoni mwa Julai.

Klabu hiyo ilitoa taarifa ikisema mabingwa hao wa Ulaya’hawatashiriki katika michezo ya kuongeza bei na ujanja unaofanywa na baadhi ya mawakala wa wachezaji.”

Kwa sasa RNSI inakabiliwa na changamoto mbili za kisheria, mojawapo ikitoka kwa winga wa zamani wa Bournemouth, Max Gradel, ambaye anadai kuwa kampuni yake ya Maxidel Management ilikuwa tayari na makubaliano na Diomande.

Gradel amewasilisha malalamiko Fifa, ingawa shirikisho hilo la soka duniani halikuzuia uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Real Madrid. Dez Bamba, ambaye ni rais wa klabu ya kwanza ya Diomande, AFI Sud Comoe ya Ivory Coast, amesema winga huyo alishawishiwa kujiunga na RNSI baada ya kupigiwa simu na Vinicius. RNSI haijatoa maoni kuhusu kesi hiyo.

Wakati huohuo, kampuni ya Rainbow World Group ilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya London na Visiwa vya Virgin katikati ya Juni dhidi ya Diomande, ikitaka ‘kutekeleza makubaliano ya kisheria kuhusu haki za picha.’Katika ulimwengu wenye ushindani mkali wa mawakala wa soka.