Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NJIA NGUMU: Yanga, Simba wakomaa Ligi ya Mabingwa Afrika

CAF Pict

Muktasari:

  • Mzunguko wa awali wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa CAF utaanza kwa mechi za kwanza kati ya Septemba 4 na 6, kabla ya marudiano kufanyika wiki moja baadaye.

CAIRO, MISRI: KUFUZU hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni miongoni mwa mitihani migumu zaidi katika soka la klabu Afrika, huku timu zikianza kampeni zao mwishoni mwa wiki hii zikilenga kufika hatua hiyo.

Mzunguko wa awali wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa CAF utaanza kwa mechi za kwanza kati ya Septemba 4 na 6, kabla ya marudiano kufanyika wiki moja baadaye.

Baada ya hapo, timu zitakutana katika mzunguko wa pili wa mchujo, ambao ndio utaamua klabu 16 zitakazotinga hatua ya makundi.

Takwimu za misimu mitano iliyopita, kuanzia 2021/22 hadi 2025/26, zinaonyesha wazi ugumu wa kufika hatua hiyo.

Katika misimu hiyo, kulikuwa na nafasi 80 za hatua ya makundi, zilizoshikiliwa na jumla ya klabu 38 tofauti.

Hata hivyo, ni klabu nne pekee zilizofuzu hatua ya makundi katika kila msimu kati ya hiyo mitano.

Klabu hizo ni Al Ahly ya Misri, Al Hilal ya Sudan, Esperance de Tunis ya Tunisia na mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kila moja ilicheza hatua ya makundi mara tano, hivyo kwa pamoja zilitwaa nafasi 20 kati ya 80, sawa na asilimia 25 ya nafasi zote zilizokuwepo.

Hilo linaonyesha jinsi ilivyo vigumu kwa timu mpya kuvunja utawala wa vigogo ambao wamejenga uzoefu mkubwa katika mashindano ya klabu Afrika.

Hata hivyo, Al Ahly haitakuwepo katika Ligi ya Mabingwa msi mu huu kwa kuwa itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo Al Hilal, Esperance na Sundowns ndizo zitakazokuwa na nafasi ya kuendeleza rekodi yao.

Nyuma ya vigogo hao kuna CR Belouizdad ya Algeria na Petro de Luanda ya Angola, ambazo kila moja imefuzu hatua ya makundi mara nne katika misimu hiyo mitano.

Belouizdad ilifika hatua hiyo katika misimu minne mfululizo kabla ya kukosa nafasi msimu wa 2025/26.

Petro, kwa upande wake, imejijengea jina kama moja ya timu zinazofanya vizuri mara kwa mara katika mashi ndano ya klabu kutoka ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Ukweli kwamba ni klabu sita pekee zilizofikisha au kuzidi mara nne za kufuzu hatua ya mak undi ndani ya misimu mitano unaonyesha jinsi ushi ndani huu ulivyo mkali na ambavyo mafanikio yana weza kubadilika haraka.


CA 02

YANGA, SIMBA, PYRAMIDS WAKOMAA

Kundi linalofuata lina klabu tano ambazo kila moja imefuzu hatua ya makundi mara tatu katika kipindi hicho.

Hapa ndipo zinapoonekana timu ambazo zimeanza ku badilika kutoka kuwa washiriki wa mara chache na kuwa sehemu ya kudumu katika hatua ya juu ya mashindano. Yanga ya Tanzania na Pyramids FC ya Misri zimefuzu hatua ya makundi katika misimu mitatu mfululizo iliyopita, jambo linaloonyesha ukuaji mkubwa wa klabu hizo katika soka la Afrika.

Kwa Yanga, mwenendo huo unaifanya kuwa miongoni mwa timu ambazo zimejijengea uthabiti katika mashindano ya juu ya klabu Afrika.

Simba SC pia imefuzu hatua ya makundi mara tatu katika kipindi hicho, ikiendelea kuonyesha Tanzania imekuwa na uwepo mkubwa zaidi katika mashindano ya CAF.

Klabu nyingine zilizofikisha mara tatu ni vigogo wa Morocco, Raja Casablanca na Wydad AC.

Hivyo, ni klabu 11 pekee zilizofuzu hatua ya makundi angalau mara tatu katika misimu mitano iliyopita.

Kwa maana nyingine, chini ya theluthi moja ya klabu 38 zilizowahi kufika hatua hiyo katika kipindi hicho zimeweza kufanya hivyo katika angalau misimu mitatu kati ya mitano.

CA 01


MAZEMBE, ZAMALEK NA WENGINE

Klabu 10 zimefuzu hatua ya makundi mara mbili katika misimu hiyo mitano.

Kundi hilo linajumuisha vigogo wenye historia kubwa katika soka la Afrika pamoja na timu ambazo zimeanza kurejea kwenye ramani ya ushindani wa juu.

TP Mazembe ya DR Congo na Zamalek ya Misri ni miongoni mwao, huku AS FAR ya Morocco na MC Alger ya Algeria zikiwa zimeanza kurejesha nafasi zao katika hatua ya makundi.

Jwaneng Galaxy imewahi kuiwakilisha Botswana na kufikisha nchi hiyo hatua ya 16 bora mara mbili, huku Sagrada Esperansa ikifanya hivyo kwa Angola.

Al Merrikh ya Sudan, Horoya ya Guinea, JS Kabylie ya Algeria na Etoile du Sahel ya Tunisia nazo zimefuzu mara mbili.


CA 05

TIMU 17 MARA MOJA TU

Klabu 17 zimefika hatua ya makundi mara moja tu katika misimu mitano iliyopita, sa wa na karibu asilimia 45 ya timu zote 38 zilizowahi kufika hatua hiyo.

Takwimu hiyo ndiyo inayotoa picha kubwa ya ushindani katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa baadhi ya klabu, kufuzu mara moja tu kulikuwa mafanikio makubwa ya kihistoria.

AmaZulu ya Afrika Kusini ilifika hatua ya makundi msimu wa 2021/22, huku FC Nouadhibou ya Mauritania ikiweka historia kwa soka la klabu nchini humo msimu wa 2023/24.

Medeama pia iliifikisha Ghana hatua hiyo katika msimu huo, wakati Stade de Abidjan ilirejesha Ivory Coast katika hatua ya makundi msimu wa 202 4/25.

Orlando Pirates ya Afrika Kusini, moja ya klabu kongwe na zilizowahi kutwaa ubingwa wa Afrika, pia ipo katika kundi la timu zilizofuzu mara moja tu katika kipindi hicho.

Hilo linaonyesha kwamba hata vigogo wenye historia kubwa Afrika wanaweza kupata ugumu wa kudumisha ubora wao msimu baada ya msimu.

Klabu nyingine zilizofuzu mara moja ni AS Maniema Union, AS Vita Club, Saint-Eloi Lupopo, ASEC Mimosas, Coton Sport, Djoliba AC, Stade Malien, ES Setif, Power Dynamos, RS Berkane, Rivers United na Vipers SC.


CA 03

TANZANIA YAJENGA NGUVU

Kwa jumla, kati ya klabu 38 zilizofika hatua ya makundi katika misimu mitano iliyopita, ni 21 pekee zilizofanya hivyo zaidi ya mara moja.

Hata hivyo, kuna dalili za kuibuka kwa nguvu mpya katika ushindani huo. Simba, Yanga na Pyramids zimefuzu mara tatu mfululizo, huku AS FAR na MC Alger zikiwa zimefanya hivyo katika misimu miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, kiwango cha juu ni klabu mbili kutoka nchi moja kufuzu hatua ya makundi katika msimu mmoja.

Kwa hiyo, kinadharia, nchi inaweza kuwa na nafasi 10 katika kipindi cha misimu mitano.

Misri ndiyo nchi pekee iliyotumia nafasi zote 10, kupitia Al Ahly mara tano, Pyramids mara tatu na Zamalek mara mbili.

Algeria na Morocco zimejaza nafasi tisa kila moja, wakati Afrika Kusini, Sudan na Tunisia zina nafasi saba kila moja.

Algeria, Morocco na DR Congo ndizo nchi zilizoingiza klabu nyingi zaidi tofauti katika hatua ya makundi, kila moja ikiwa na klabu nne.

Misri na Afrika Kusini zimewakilishwa na klabu tatu tofauti.

Takwimu hizo zinaonyesha wazi kwamba ushindani wa kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hauishii kwenye ukubwa wa jina la klabu; uthabiti, uzoefu na uwezo wa kushinda mechi za mchujo ndiyo huamua nani atafika kwenye meza ya vigogo 16.