Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE WA UPUPU: Gerrard Pique alipopita njia ya Juma Nature

NANI anakumbuka penzi la Juma Nature na Sinta mwaka 2003? Ni mapenzi yaliyotikisa nchi katika zama ambazo hakukuwa na WhatsApp wala Instagram. Habari za mastaa utazipata kwenye magazeti ya udaku tu. Juma Nature alikuwa staa mkubwa sana wa BongoFlava na Sinta alikuwa staa mkubwa sana wa BongoMovie. Tasnia hizi mbili ndizo zilizokuwa zikiwindwa na magazeti ya udaku.

Bahati mbaya ni kwamba penzi hilo lilikuja na kuondoka na upepo, na baada ya kuvunjika, Juma Nature aligeuza mkasa wake wa mapenzi na mrembo huyo kuwa pesa.

Allitoa albamu iliyoitwa ‘Ugali’ iliyokuwa na nyimbo nne zilizozungumzia mkasa wa penzi hilo, na zote zilibamba sana ambazo ni Sitaki Demu, Sitaki Demu Remix, Inauma sana na Inaniuma sana Remix Inaniuma sana ulikuwa na dakika nane...yes, ni nane. Kwa hizi nyimbo za sasa, unapata nyimbo tatu ndani yake.

Siku ya uzinduzi wa albamu hii, Juma Nature alijaza Ukumbi wa Diamond Jubilee na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo. Albamu hiyo iliuza nakala nyingi sana, japo ni bahati mbaya sana kwamba wakati huo hakukuwa na mifumo mizuri ya kujua idadi kamili.

Kupitia mauzo ya albamu hiyo, Nature alinunua gari aina Mark II mpya, ikapata ajali na akanunua nyingine hapo hapo, famasikhara nini!!

Unaweza kuona kama masihara ukiizungumzia Mark II kwa sasa, kipindi ambacho wakina Diamond Platinumz wanatembelea magari ya kifahari kama Rolls Royce na Cadillac Escalade.

Nature alikuwa habari ya mjini na Mark II yake. Kwa kifupi, Juma Nature aligeuza matatizo ya penzi lake na Sinta kupiga hela...na akapiga kweli kweli.

Na hiki ndicho anachokifanya Gerard Pique, nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania. Pique aliangukia kwenye penzi la mrembo wa Colombia, Shakira, tangu walipokutana kwenye Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Pique alikwenda na timu yake ya taifa na Shakira alikwenda na wimbo wake wa WAKAWAKA...This time for Africa.

Wakati huo Shakira alikuwa akitoka kimapenzi na Antonio de la Rua, lakini akamtosa kwa ajili ya staa Pique, kijana mdogo wa miaka 23 na Shakira akiwa mama wa miaka 33.

Penzi likaenda mbali na kugeuka ndoa iliyoleta duniani watoto wawili wa kiume, Milan na Sasha.

Lakini majira ya baridi mwaka jana, ikabainika kwamba Pique alikuwa akitoka kimapenzi na binti ‘mchanga’ wa miaka 22, Clara Marti.

Habari ilikuwa msumari wa moto kwenye moyo wa Shakira ambaye alijaa gesi na kuomba talaka.

Masikini mama wa watu alipaniki kiasi cha kutunga wimbo maalumu kwa kumpiga kijembe binti huyo.

Wimbo huo unaoitwa BZRP Music Sessions, umeimbwa kwa ushirikiano na Prodyuza kutoka Argentina, DJ Bizarrap.

Ndani yake Shakira anasema,

I am worth 22. You traded a Ferrari for a Twingo, you traded a Rolex for a Casio. Nina thamani ya (wanawake) wawili (wa miaka) 22.

Umebadilishana Ferrari na Twingo, umebadilishana Rolex na Casio. Shakira ana miaka 45 sasa kwa hiyo anaposema ana thamani ya wanawake wawili wa miaka 22, anamaanisha yeye ni sawa na akina Clara wawili.

Halafu anaposema ‘unabadilishana Ferrari na Twingo’, anamaanisha gari aina ya Reanult Twingo, ambayo ni ya thamani ndogo sana, yaani kama IST. Kwa hiyo yeye ni Ferrari na Clara ni Twingo.

Na anaposema ‘unabadilishana’ Rolex kwa ajili ya Casio, anamaanisha yeye ni sawa na Rolex, saa ya bei mbaya sana na Clara ni Casio, saa ya kimulimuli.

Lakini Pique ni kama kamgeuzia sikio la nyuma kwa sababu baada tu ya wimbo huo kutoka, Pique akaenda kununua Twingo yake na akaanza kuitembelea mitaani.

Lakini hakuishia hapo, Pique akataka kupiga hela kupitia mkasa huu wa mapenzi, kama Juma Nature alivyopiga hela kwenye mkasa wa penzi lake na Sinta.

Pique ana mashindano yake ya soka la watu sita sita yanayoitwa Kings League yanayofanyika kwa kuwahusisha wachezaji mbalimbali wa sasa na zamani.

Baada ya wimbo wa Shakira, akapata udhamini mnono kutoka kampuni ya saa ya Casio, ile aliyoipondea Shakira.

Shakira alikesha kutunga mashairi ili kumkomoa Pique na Clara wake, kumbe ndiyo amempa mchongo wa pesa ili aendelee kutanua na kimwana huyo.

Shakira mwenyewe ambaye alikuwa akiishi na mumewe Pique mjini Barcelona, kaamua kuhama kabisa hadi bara, siyo mji au nchi tu...yaani kahama bara kabisa.

Kwa sasa kahamia Miami, Florida Marekani, ili awe mbali na walimwengu...maana asije akaendelea kuwatengenezea pesa.