Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtasingwa hana cha kujitetea Kaizer Chiefs

MTASINGWA Pict

Muktasari:

  • Huu usajili umewakosha wengi hapa kijiweni kwa sababu tatu kubwa na za msingi kabisa ambazo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana nazo.

JUMANNE ya wiki hii, kiungo wa mpira, Adolf Mtasingwa alikamilisha uhamisho wa kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini akitokea kwa wauza aiskrimu, Azam FC.

Huu usajili umewakosha wengi hapa kijiweni kwa sababu tatu kubwa na za msingi kabisa ambazo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana nazo.

Kwanza Azam FC imevuna mzigo wa kutosha ambapo inatajwa kwamba imepata kiasi cha Dola 500,000 (Sh1.3 bilioni) kutokana na mauzo ya mchezaji huyo.

Pili mchezaji mwenyewe naye ataboresha kwa kiasi kikubwa maisha yake kwani kijiwe kimenasa habari za ndani kwamba atalipwa mshahara wa Dola 30,000 (Sh79 milioni) kwa mwezi.

Jambo la tatu ni kwamba anakwenda katika ligi yenye ushindani zaidi ambayo itamtengeneza awe mchezaji bora zaidi na atakayekuwa msaada kwa timu yetu ya taifa, Taifa Stars.

Kwa kule Afrika Kusini, kijiwe kina imani kubwa kwamba Adolf Mtasingwa atatoboa kwa maana ya kufanya vizuri kwani hana kinachoweza kumpa tabu kuishi huko.

Kwanza ni mchezaji msomi na anayefahamu vyema lugha ya Kiingereza inayotumika kule, hivyo haiwezi kuwa changamoto kwake tofauti na iwapo angekuwa hafahamu lugha hiyo.

Lakini jambo lingine linalotuaminisha ni kwamba Mtasingwa ana uzoefu mkubwa wa kucheza na mazingira ya mbali na nyumbani Tanzania, hivyo hatokuwa na woga huko Afrika Kusini.

Kama aliweza kucheza nje ya Tanzania akiwa bwana mdogo katika nchi za Sweden na Finland, hawezi kushindwa hapo kwa Madiba.